TUGUTUKE VIJANA MUDA BADO UPO - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 9 November 2017

TUGUTUKE VIJANA MUDA BADO UPO

Nimejaribu kufatilia video ya mahojiano kati ya millard ayo na Mzee salum Sumry,nikajikuta napata la kuandika leo hii. Nimewaza mengi sana japo interview ilikuwa fupi lakini nilipata majibu na maswali mengi sana, hii ilinifanya nikubali kumaliza MB zangu kuangalia mara mbili mbili kabla sijapata wazo la kui download hiyo video tokea YouTube.

Ukiangalia yale mahojiano utajifunza mengi sana ila kwangu mimi ambaye napenda biashara ningependa nibakie upande wa biashara.

Katika maelezo yake mzee Sumry amesema kuwa Biashara ya mabasi ina changamoto nyingi sana then akasema zipo ambazo zinaepukika nyingine zinavumilika. Akaja sema changamoto kubwa sana inakuja kwenye management na kwenye competition.

Tukiongelea katika utawala au uendeshaji wa kampuni kaeleza kuna shida ya madereva hasa kuliko wengine then akaja gusia kuhusu wahusika wa mahesabu kuwa wanapigia mahesabu mafuta tu katika basi hawaangalii kama kuna changamoto nyingine zaidi ya mafuta katika uendeshaji wa magari.  Kwa maana hiyo akaamua kuuza magari yote na kujikita katika KILIMO. haya ni maamuzi ya kishujaa kwa tajiri mkubwa kama Mzee Sumry.

Kwa nn ameamua kuingia kwenye kilimo badala ya kwenda kwenye biashara nyinginezo. Ni kwasababu ameona fursa kama alivyo jieleza kuwa ameingia kwenye kilimo kwa kuona fursa kubwa iliyopo ambapo Tanzania kilimo ndio mhimiri wa taifa katika uchumi lakini kidunia ni daraja la nne katika vyanzo vya maendeleo katika nyanja za ujasiriamali. 

Je mimi na wewe tunalijua hilo, je tuko tayari kuacha biashara tulizonazo ambazo zinatuingiza kidogo tukaingia kwenye kilimo.

Kwa hiyo akaelezea pia alianza na kiasi gani cha eneo na faida alipopata akaja lima tena kiasi gani na mwaka huu ameelezea nini target yake katika ukubwa wa eneo. Kwanini sisi tusiamue leo kama vijana wenye chachu ya mafanikio.

Ok, niongelee changamoto alizokutana nazo mwaka huu, moja ya changamoto kubwa ni kuzuiwa kwa wakulima kuuza vyakula nje ya nchi ili hali wa nje wanaleta ndani ya nchi. Hizi ni changamoto ambazo tunatakiwa tuzielezee kwa viongozi wetu ili wazitatue mapema kwa lengo la kukuza pato la mkulima na pato la taifa kwa ujumla..

Lakini kutokana na changamoto hizi sisemi kuwa itatufanya tushindwe kulima au kupata faida baada ya kulima ila itapunguza ukubwa wa faida na kutufanya tupate kipato cha chini ya malengo tulio jiwekea...

Ila kumbuka kaingiza mashine ya kuvunia mazao bureeeee bila riba wala makato yoyote ya nchi, hii ni fursa kubwa kwetu sisi vijana kuagiza vifaa vya kutusaidia mashambani kutokea nje kwa bei ndogo na tukaweza kulima zaidi. Sina uhakika kwa trekta kama zinaingizwa nchini bure ila nitafatilia hili

Nini nawashauri vijana wenzangu, ni kuwa tuamke, tuamue kujikita katika kilimo biashara, tutafanikiwa zaidi ya tunavyowaza ndani ya ajira.

Kila tajiri mkubwa duniani utakuta amewekeza katika kilimo hata kama utajiri wake umeshikiliwa na biashara nyingine.

Let's wake up, tupambane, TUTAFANIKIWA.

It's SHAFIINAD

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here