NDOA NA MAFANIKIO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 7 September 2017

NDOA NA MAFANIKIO.Habari, leo napenda niongelee mada ya ndoa na pia mafanikio, Nimemua kuyaandika haya kwa sababu kuna watu wanachanganya sana maneno kuhusu ndoa.

watu wanaamini ndoa au ukitaka kuoa ni mpaka uwe na mafanikio, hapana ndoa ni njia moja wapo nzuri na rahisi ya kufikia mafanikio.
Ndoa ni nguzo moja wapo ya mafanikio na ndio nguzo ambayo Mungu huibariki na kuleta mafanikio haraka ndani yenu.

Ndoa ikiwa nzuri yenye amani huleta mafanikio ndani, unaweza ukahangaika miaka 10 ya kujitafutia maisha bila ndoa ukaona ugumu mkubwa mbele yako ya mafanikio, lakini ukioa tu unakuja ona mafanikio ghafla. usije sema ndio muda umefika wa mafanikio ila ni kwa sababu Umepata mwenzako ambaye anakusaidia katika kufikia malengo na huyo mwenzako ndio nguzo yako na ndio msaada wako katika kufikia malengo yenu.

Umoja ndio nguzo yenye kuleta mafanikio haraka, maelewano na upendo ndio huleta maendeleo ndani ya nyumba yenu.

Kwanini kijana uogope kuoa au kuanza maisha ya ndoa? kuna faida kubwa sana ukiishi maisha ya ndoa na moja ya yote ni mafanikio ya kiuchumi na kiroho pia.

Napenda nitoe mfano wa ndoa ambao nili hadithiwa na profesa wangu.

"Siku moja jioni akiwa amekaa na familia yake nyumbani, alikuja mama mmoja ambaye ni jirani yake na alipofika alimwita mke wa prof. na kumuambia kuwa amevuna mpunga na angependa ampe gunia moja mke wa Prof. ili akakoboe na ale na familia yake.
basi akapewa hilo gunia na walikula miezi miwili ndio wakamaliza,".

Nini cha kujifunza hapo..?
Ni kuwa angekuwa prof peke yake kwanza asingepata mtu wa kuja kumpa kwa maana angekuwa peke ake na pia mke wa mtu angesema tu anakuja pale angeonekana anachepuka nae.
pili prof. asingeweza kuzoeana na majiran kama mkewe alivyozoeana na majirani zake mpaka akapewa hilo gunia.

Na mengineyo mengi, kwa hiyo ninaposema Ndoa inaleta mafanikio, Sibahatishi namaanisha. Nawashauri vijana wenzangu tujitoe, Tuache uoga wa kusema hatujajipanga katika ndoa.
maisha ya ndoa yana faida na ndio njia moja wapo ya kupata mafanikio kwa haraka kwa maana mtakuwa watu wawili ambao mnataka mafanikio ya aina moja kwa pamoja.

Wanasema "MWANAMKE MZURI, ANALETA USAWA KATIKA MAISHA YA MWANAUME".

nakutakieni mafanikio mema.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here