JE? KUNA UHUSIANO KATI YA UPOTEVU WA NYWELE KICHWANI (KIPARA) NA NGUVU ZA KIUME? - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 12 September 2017

JE? KUNA UHUSIANO KATI YA UPOTEVU WA NYWELE KICHWANI (KIPARA) NA NGUVU ZA KIUME?

Uhusiano kati ya testosterone na upotevu wa nywele kichwani (kipara) ni mgumu sana kuulezea, Baadhi ya watu huamini kuwa watu wenye vipara wana level ya juu ya hormone hii, swali je ni kweli? Kuna ukweli juu ya hili…?
Upotevu wa nywele unatokana na kusinyaa kwa hair follicle na kusinyaa huku kunaleta shida katika mzunguko wa ukuaji wa nywele, Nywele mpya zinakuwa laini na laini mpaka kunafikia nywele hazioti eneo hilo na follicles zinakuwa dormant. Na hili tatizo linasababishwa na hormones na baadhi za genes.

MIUNDO TOFAUTI YA TESTOSTERONE HORMONE
Testosterone zipo katika mwili wako katika mifumo tofauti tofauti, Kuna “free” testosterone ambazo hazijawa bounded na proteins katika mwili wako, na hii ndio form ya testosterone ambayo inapatikana sana katika mwili wetu.
Pia kuna Testosterone ambazo ziko bounded na albumin, (protein ndani ya damu).
Na pia testosterone nyingi ziko bounded na  hormone za jinsia yaani sex hormone-binding globulin (SHBG) protein na pia haiku active. Kama una kiwango cha chini cha SHBG, unaweza kuwa una kiwango cha juu cha free testosterone katika mzunguko wako wa damu.
Dihydrotestosterone (DHT) inatengenezwa kutoka kwenye testosterone na enzyme inayojulikana kama 5-alpha reductase, pia inaweza tengenezwa na DHEA (hormone maarufu kwa wanawake) . DHT ina nguvu mara tano zaidi ya testosterone. DHT primarily inatumika na mwili katika korodani, ngozi na  hair follicles. Actions ya DHT na usensitivity wa  hair follicles kwenye DHT ndio sababu ya upotevu wa nywele kichwani.
DHT pia ipi kwenye korodani.  Bila  DHT, korodani hazitakuwa vizuri kama zinavyotakiwa ku develop. Lakini pia kuwa na DHT nyingi zaid kunaweza pelekea mwanaume kupata benign prostate hypertrophy, pia inajulikana kama uvimbaji wa korodani yaani (an enlarged prostate).
Ni genes zako.
Sio kiwango cha testosterone au DHT ambayo inasababisha kipara.; ila ni sensitivity ya hair follicles zako. Na hiyo sensitivity inaangaliwa kwa genetics. AR gene inatengeneza receptor katika hair follicles ambazo zitaingiliana na testosterone na DHT. Kwa hiyo kama receptors zako ni sensitive, itakuwa rahisi zaidi kuwa triggered na hata kiwango kidogo cha DHT, na pia upotevu wa nywele utatokea kiurahisi zaidi. Pia genes nyingine zinaweza changia.
Pia Umri, mawazo na sababu nyingine zinaweza changia ukapata upotevu wa nywele lichwani, ila genes ndio zinachukua nafasi kubwa ya visababishi vya hili jambo.
Upotevu wa nywele kwa wanawake.
Wanawake pia wanaweza pata hili jambo la upotevu wa nywele kichwani ambapo huweza sababishwa na androgenetic alopecia. Ingawa wanawake wana kiwango kidogo cha testosterone kuliko wanaume,  lakini zinatosha kusababisha androgenetic hair loss.
Kuna dawa zinapatikana katika hili jambo.
Njia nyingi zapo za kutibu hii shida upotevu wa nywele kwa wanawake na wanaume na dawa hizo zinafanya kazi ya ku interfere kazi za testosterone na DHT. 
Finasteride (Propecia) Ni dawa inayozuia 5-alpha reductase enzyme ambayo ina converts testosterone kwenda DHT. Ni hatari kutumika kwa mama mjamzito au anayetegemea kuwa mjamzito, na pia ina madhara kwa wote katika tendo la kujamiiana.

Na inhibitor nyingine inayoweza zuia 5-alpha reductase inaitwa dutasteride (Avodart) ni dawa inayopatikana sokoni kwa ajili ya kutibu uvimbaji wa korodani,
Lakini pia kuna dawa nyingine zinazohusika kutibu bila kuingilia mfumo wa utendaji wa testosterone na DHT: ni hizi hapa chini.
Ø  minoxidil (Rogaine)
Ø  ketoconazole
Ø  laser treatment
Ø  surgical hair follicle transplant


No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here