Njia 5 za mitandao ya kijamii zinaweza kukuza biashara yako. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 6 August 2017

Njia 5 za mitandao ya kijamii zinaweza kukuza biashara yako.Mitandao ya kijamii ina msaada mkubwa sana kwa watu wanaomiliki biashara. Na ukuaji wa mitandao ya kijamii sasa inakuza zaidi biashara mfano Twitter, Facebook na LinkedIn, kinachotakiwa ni wewe kujua hii mitandao na mbinu za kuwa na uwezo wa kukuzia biashara zako kupitia mitandao hii ya kijamii.
Hapa leo nakuandikia njia tano za kuweza au kukusaidia wewe ku save muda wako na kupata kutambulika mahali pakubwa duniani, na pia utapata followers wengi na utapata mafanikio mazuri.

Andika vitu vipya.
Kama utapost makala ambazo zimeandaliwwa hivi karibuni na zinauhusiano na dhana yako na pia ikawa ni muhimu kwa watu wanaokufuata, itakuwa safi na itawafanya wale wanaokufatilia kuendelea kukufatilia na kutembelea zaidi website yako.

Mitandao ya kijamii inaongea Lugha mpya.
 Na lugha ninayosemea hapa ni lugha ya picha, video na maandiko (makala). Hizi aina za mitandao zinakuza sana biashara katika zama hizi, lakini biashara ni zile ambazo zinajikita katika kutangaza biashara zao kupitia mitandao hii ya kijamii.
Lugha hizi unaweza zitumia mwenyewe inategemea na nini unataka watu wako wakione au wakisome.

 

Kuza upatikanaji wako.
Kuwafikia followers, subscribers na marafiki ni uti wa mgongo wa mafanikio ya biashara yako kupitia mitandao ya kijamii. Na njia kuu na nzuri ya kupata wateja wako wapya ni kurusha matangazo kupitia mitandao hii ya kijamii mfano   Facebook au Twitter ni njia ya kuongeza likes na followers, lakini pia unakuwa una promote blog yako au kutengeneza offer zaidi na watu kuziona.

Okoa Muda.
Muda siku zote ni mali, na kama ni mjasiriamali maana yake unatakiwa kufanya kazi ya uzalishaji kwa  muda mwingi sana, kwa hiyo kukaa kwenye mitandao ni moja ya njia itakayo kulazimu upoteze muda mwingi sana. Kwa hiyo mitandao ya kijamii ikaliona hilo na ikakuletea njia mbali mbali mfano. Unaweza andika makala zako ukaziweka facebook na ukazipangia muda na siku za kuwa published na kwa maana hiyo unaweza panga maandiko yako ya mwezi ukaweka humo na zenyewe zikajipost muda ukifika.
Pia kuna njia ya auto responder pale mteja anapotuma meseji kutaka kupata ufahamu wa biashara yako, auto responder inakusaidia wewe kumueleza mteja wako either asubiri jibu au kama haupo hewani kwa muda huo, inategemea na wewe utakavyotaka wateja wako wapate ujumbe wa aina gani. 

Kuwa chachu ya mabadiliko na kuwa na ujuzi zaidi.
Wakati mitandao ya kijamii ikibadilisha miongozo yao, wewe unakuwa na nafasi mbili. Unaweza kuyakubali mabadiliko na kuyaendeleza au unaweza ukaachana nayo kwa kushindwa kubadilika. Utakapojipa wazo la kukomaa na kuendelea na mabadiliko hayo, unajipa nafasi ya wewe kuchukua nafasi za wale wote ambao waliacha au walikata tama na mabadiliko hayo.
 
Mfano hivi karibuni facebook wamezuia utangazwaji wa washindi walioandika makala zaidi. Hii ingawa kwa sasa watu wameanza kuizoea lakini mwezi huo huo LinkedIn walianzisha mfumo wa kufungia profile ambazo huzitaki au meseji ambazo huzitaki, hii ni direct inawanufaisha watu kwa maana itapunguza sana spam sms na vinginevyo. Kwa hiyo mitandao hii inapobadilika na sisi tunatakiwa tuzidi kuanzisha zaidi vitu vipya kupitia mitandao hii.

Lakini wakati mitandao ya kijamii ikiendelea na faida za kuifanya biashara ikue zaidi, watu wale wanaopenda kujifunza na kushuhudia kwa matendo ndio watu ambao wanajikuta wanafanikwa zaidi.
Mjasiriamali anaweza akawa busy na kujikuta akisahau kuandaa au kutengeneza mawazo mengine zaidi kila week, fanya malengo ya kufikiria katika kubadili na kunyanyua biashara zako na mafanikio yako kupitia mitandao hii.

Endelea kuwa nasi katika blog hii na tutazidi kukuandikia zaidi pale tunapoona lina umuhimu katika maendeleo yetu sisi vijana na wajasiriamali kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here