KWANINI NAAMINI BIASHARA YA CHAKULA NA AFYA KULIKO BIASHARA NYINGINE. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 11 August 2017

KWANINI NAAMINI BIASHARA YA CHAKULA NA AFYA KULIKO BIASHARA NYINGINE.Habari za muda huu ndugu msomaji wa makala zangu, Leo napenda niongelee kwanini huwa naamini sana kufanya biashara za kilimo (chakula) na afya kuliko biashara nyingine.?
kwa kuanza tu ningependa kusema kuwa nikifanyacho mimi ni kile ninachoamini na kukiona nakiweza kwa hiyo usichukulie kauli yangu kuwa biashara nyingine hazifai, hapana zinafaa ila nina elezea biashara ninazopenda kuzifanya.

kwa hiyo hapa chini nitatoa faida za biashara za chakula na afya then kwa kuzigeuza utapata hasara katika biashara tofauti na hizo.

Biashara ya chakula na afya ni ya uhakika kwa sababu ni lazima binadamu atakula na pia akiumwa lazima atakuja umpatie dawa na matibabu, kwa maana hiyo utakuwa na uhakika wa kuuza kila siku na kila siku utapata faida kidogo itakayokufanya biashara yako izidi kukua na kuona faida yako.

Then biashara ya chakula hupanda bei haraka zaidi na faida kuwa kubwa karibu kila mwaka, Haitegemei fashion, Biashara hii unaweza kujituma mwenyewe ukalima then ukaja uza bei ikipanda au ukanunua wakati watu wanavuna ukaja kuuza bei ikipanda. na afya mifano tunayo mingi pharmacy zinavyolipa mitaani.

simaanishi kuwa biashara nyingine hazilipi, hapana biashara nje ya nilizotaja zinalipa ila kwa ushauri wangu kama unamtaji unaweza anzisha biashara hizi. unaweza ukawa unalima mwenyewe then ukivuna unauza kwa kusubiri bei ipande na unapat kipato kizuri tu. Au unaweza ukafungua Maabara, Pharmacy au Dispensary kama una huo uwezo na ukajipatia pesa nyingi na kwa urahisi lakini kama utatoa huduma nzuri, bora na za uhakika maana sekta ya afya haihitaji mtu anayetanguliza pesa, ila kama utatanguliza afya kwanza ndio faida kubwa utaiona hapo baadae.

Kilimo ni njia rahisi kwa sisi tusiokuwa na mitaji, kwa maana ukiamua kujituma mwenyewe shambani ukahusika sehemu kubwa, utajikuta umepunguza gharama za kulimiwa na watu na wewe utajikuta umetumia mtaji kidogo na faida kubwa na Kumbuka faida hii utakayopata wakati wa mavuno ni pesa ambayo haitakuwa inahusika katika matumizi ya yaliyopita.

mfano mfanyakazi anayepokea laki 5 kila mwezi sio sawa na mkulima anayepata milion mbili kila akivuna. Tofauti yao ni kuwa mfanyakazi ile laki tano anaingiza katika matumizi ya nyumbani, mafuta ya gari, Umeme na vitu vingine. Ila mkulima mpaka aje kuvuna atakuwa kesha maliza muda wake wa nyuma ambao alihangaika na ukapita. kumbuka mkulima anajiwekea chakula na atanunua vitu vichache sana. na hiyo milion mbili atakuja ishika kwa mara moja wakati mfanyakazi anapata kidogo kidogo.

Lakini kama mfanyakazi akilima atafanikiwa haraka sana kuliko mkulima asiye na kipato cha ziada.

Kama utapenda nikupatie elimu ya namna ya kulima au Kufungua maabara, pharmacy au Dispensary unaweza nitumia sms katika facebook page yangu ya Shafii Said Rajabu au Shafiinad blog pia zote nitakujibu.
pia unaweza nicheki kwa e-mail:- shafiikuku@gmail.com.
karibu sana shafiinad.com upate maarifa.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here