KILIMO CHA FENNEL NA MATUMIZI YAKE KIAFYA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 20 August 2017

KILIMO CHA FENNEL NA MATUMIZI YAKE KIAFYA


Utangulizi
Fennel ni mmea wenye asili ya ulaya kusini na maeneo ya Mediterranean, ambao hulimwa zaidi kwa ajili ya ladha yake ambayo hutumika katika vyakula mbalimbali na matibabu.
Nchi zinazolima zao hili ni pamoja na nchi za India, China, Argetina na Indonesia.

Umbile la mmea 
Fennel ni mmea wenye majani yenye rangi ya kijani iliyokolea iliyochanganyika na kijivu. Mmea huu una harufu kali katika sehemu zote za mmea isipokua mizizi.
Mmea una urefu wa upatao mita moja na nusu.


Uzalishaji
Fennel hustawi vizuri katika maeneo yenye nyuzi joto kati ya sentigrade 4 hadi 27, na mvua za wastani wa milimita 30 hadi 260 kwa mwaka. Udongo wa tifutifu unafaa zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

Zao hili huoteshwa kwa kutumia mbegu ambazo huoteshwa katika kina cha nusu inchi katika mistari iliyo katika umbali wa futi moja ambapo nafasi kati ya mmea na mmea ni inchi 6.

Mmea wa fennel huweza kuanza kuvunwa majani machanga baada ya miezi miwili tangu kupandikizwa. Pia mmea huu huweza kuendelea kuvunwa kwa mwaka mmoja hadi miwili.

Fennel hutoa mbegu kila mwaka. Yafaa mbegu zivunwe mapema kabla hazijakauka sana kwani hupukutika kwa urahisi.


Matumizi
Fennel ni mmea ambao una mafuta yenye kemikali za enethole, dfenchone, methyl chavicol, feniculum, naanisic acid
Kemikali hizi na zingine hufanya fennel kutoa harufu na ladha nzuri katika vyakula mbalimbali.

Mbegu za fennel hutumika katika vyakula vya nyama, mboga, samaki,
salad, mikate, chai, na vinywaji vikali. Mafuta aina ya oleoresin yaliyomo katika fennel hutumika katika utengenezaji wa peremende, sabuni, manukato na vipodozi.

Majani machanga hutumika zaidi katika vyakula mbalimbali.
Fennel ni mmea ambao pia hutumika katika matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukohoa, ngiri, kuvimbiwa, maumivu ya tumbo, na kusisimua utoaji maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha.

Kwa kifupi, hili ni tunda linalotumika sana kiafya. na linalimika tanzania na lina soko zuri tu.

Karibu shafiinad tujifunze zaidi.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here