NAMNA YA KUUNGANISHA INTERNET KUTOKA KWENYE SIMU KWENDA KWENYE COMPUTER. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 14 August 2017

NAMNA YA KUUNGANISHA INTERNET KUTOKA KWENYE SIMU KWENDA KWENYE COMPUTER.


Habari wana shafiinad blog, leo tuone kwa ufupi kidogo juu ya teknolojia ya kuunganisha mtandao wa internet kutokea kwenye simu kuja kwenye computer. Hii ni teknolojia ambayo imepunguza sana matumizi ya moderm mtaani na watu kutumia simu zao kama ndio moderm na kuweza kupata mtandao wa internet kwa speed nzuri na zaidi ya ile ya moderm.

Kwa hiyo leo hapa nitazungumzia njia mbili ambazo hutumika katika kuunganisha mtandao wa internet kutokea kwenye simu kuja kwenye computer. ambazo ni Wi-fi Hotspot na Usb Tethering.

Tukianza na Wi-Fi Hotspot ni njia ambayo ni wireless yaani bila kuchomeka waya wowote. njia hii inatumia mawimbi ya internet kutokea simuni mpaka kwenye kifaa cha pili kinaweza kuwa computer au simu nyingine.
Hatua ya kwanza ni kujua namna ya kuwasha hiyo hotspot na hapa ningependa niongelee zaidi simu za android.

Unatakiwa uende setting>more>portable hotspot then unaiweka on.
kama picha hapa chini inavyoonekana.
 kisha washa hotspot yako na baada ya hapo utaenda kwenye simu yako utawasha Wi-fi ya kawaida au kama picha hapa chini inavyojieleza.. na kwa computer utabofya sehemu ya icon pale inapokaa alama ya betri ikiwa imewashwa... kuna sehemu ya mtandao ukibonyeza hapo kama simu yako ina drive ya kupata mawimbi ya Wi-Fi hotspot itanasa na kuanza kupata mawimbi ya mtandao wa internet.

Kumbuka kuna baadhi ya device Wi-Fi hotspot yake imefungwa kwa namba za siri yaani password na wakati wa kuunganisha kwenye simu au computer yako itahitajika uiweke hiyo paasword.

jinsi ya kujua hiyo password utaenda mpaka kwenye Wi-fi hotspot then kwa kufata picha hapa chini utaona ninachosema...
 
baada ya hapo utaingia neno Set-up Wi-Fi Hotspot na hapo utafika sehemu ya password yako na utaweza badili jina na namba za siri pia au ukamua kuacha zilizopo...
na hapa nimeongelea kuhusu Wi-Fi Hotspot na katika makala yangu ijayo nitaongelea namna ya kuunganisha kwa kutumia Usb Tethering. 

Karibu na share na marafiki zako ili waweze kupata ujuzi huu...
Karibu shafiinad blog kwa mafunzo mengi ya ujasiriamali, afya na technolojia kama hizi.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here