KWANINI WATU WENGI WAMEJITOLEA KUANDIKA MAKALA ZA UJASIRIAMALI WAKATI WAO UTAKUWA HAWANA HAYO WAYASEMAYO.? - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 13 July 2017

KWANINI WATU WENGI WAMEJITOLEA KUANDIKA MAKALA ZA UJASIRIAMALI WAKATI WAO UTAKUWA HAWANA HAYO WAYASEMAYO.?
Leo nataka tujikosoe sisi ambao tunaandika makala nyingi juu ya ujasiriamali na motisha ya namna ya kuweza kufanikiwa wakati sisi tunaonekana wengi wetu tuna maisha ya kawaida ambayo hayaendani na kile tunachokisema kila siku...

Kuna mtu mmoja aliwahi niuliza hivo kuwa ni kwanini watu wanaotoa mafunzo hawana uwezo huo wanao uongelea kila siku..

Na mimi nikawaza kweli kabisa kuwa tupo baadhi (Siwezi kujitoa sababu sijafikia pale ninapopataka) ambao hatuna maendeleo ya kiuchumi kama tunavyoongelea kila siku ila napenda mjue kuwa kuna maana kubwa sana katika mafanikio ya kiuchumi..

Ningependa nielezee zile chache ambazo mimi nazifahamu ili angalau tupate mwanga ni kwanini wengi wa wanaoandika makala hizi hawana uwezo mkubwa wa kifedha wanao usema kila siku...

Maana ya kwanza ya Mafanikio ni:-
 
Kufikia lengo lako la maisha.- hapa ndipo kila kitu huwa kinahesabika kama mafanikio, Mimi mfano sio kweli ninawaza nikiwa na blog ambayo nitakuwa naandika makala za ujasiriamali na kuwafikia watu zaidi ya mia (100) kwa siku ndio itakuwa moja ya mafanikio maana ndio lengo langu basi amini ukifikia hapo na wewe utajiona umefanikiwa maana utahitajika ujifunze kuhusu blog, Internet na vingine vingi ambavyo vitakufanya uhangaike kufikia malengo yako ya kuwa na blog, Hivyo hivyo kwenye maisha ukifanikiwa kufikia lengo lako basi umefanikiwa..

Lakini pia kuna maana ya pili ambayo ni:-
Kutoka pale ulipokuwa na kuwa na kipato zaidi.- Unaweza usiwe na lengo la kufanikiwa ila ukajikuta umetoka katika hatua ya kula mlo mmoja na kujikuta ukila milo mitatu kwa siku, haya ni mafanikio ya kutoa ushuhuda wa mafanikio yako maana tokea mlo mmoja mpaka mitatu kuna changamoto nyingi umezipitia ambazo zilikukatisha tamaa na kwanamna moja ama nyingine wapo wengi ambao wanahitaji kufanikiwa na wapo kama wewe ulivyokuwa. kwa kuwaelezea itawasaidia na wao watafika hapo ulipo.

Pia kwa maana nyingine ya mafanikio kwa mtu ni ile hali ya kuwa huru katika kipato chake kifedha na hata kielimu na hii ndio wengi hukuta tunaangalia baada ya kuambiwa mtu huyu ana mafanikio.
Wengi tumekuwa na tabia ya kutaka kujua kama mtu mwenye mafanikio anatakiwa awe ni mtu mwenye kipato kikubwa cha pesa, Awe ana gari nzuri ya bei, Awe ana nyumba nzuri ya kisasa na Mambo mengine ya starehe. Lakini hii sio maana kuu ya mafanikio ya mtu.

Mafanikio ya mtu huja katika njia tofauti, Kila mtu anafanikiwa na tofauti ni mafanikio ya aina gani.
Mimi huwa napenda kusisitiza watu wajitume, wapambane na waweke juhudi juu ya kile wanachokifanya nikiamini fika kuwa bila wao kupambana na kukomaa na kile wanachoamini hawataweza pata MAFANIKIO maana mafanikio huhitaji Akili, Nia, Uwezo wa kubuni njia na Utayari wa kulifanya hilo jambo ili ufanikiwe...

Kwa maana hiyo Naweza kusema na mimi ni miongoni mwa watu waliofanikiwa 😜😜 maana nina Blog ninayotoa yale mawazo yangu ya ujasiriamali...

Usicheke ni moja ya malengo 1000 niliyojiwekea humu duniani likiwemo la KUMUABUDU MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI. na hili ndio lengo kuu kwa kila mwanadamu aliyoko duniani...
kwa hiyo kila mmoja wetu ana sababu zake nyingi za kusema amefanikiwa.

Usimsahau Mungu wako. yeye ndio mpaji kwa kila jambo hapa duniani.

napenda kuhitimisha makala hii ila kwa mwenye swali, Mwenye Wazo au ushauri juu ya mada hii usiiste kuweka comment yako hapa chini.

Pia share link na wengine ili wengi waweze kuona na kujua ama kupata majibu ya kile walichokuwa wanajiuliza juu ya mada ya leo.

karibu shafiinad uweze kusoma na kupata motisha ya kufanya ndoto zako ziishi.

ISHI NDOTO YAKO.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here