UONGOZI HAUANGALII UKUBWA, UNAANGALIA UJUZI,UJASIRI NA BUSARA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 2 July 2017

UONGOZI HAUANGALII UKUBWA, UNAANGALIA UJUZI,UJASIRI NA BUSARA


KIONGOZI HUWA NA BUSARA NA MAWAZO CHANYA

Habari za muda huu wana jamii wenzangu, wasomaji wenzangu wa shafiinad. leo nimeona tuongelee japo kwa ufupi uongozi ambao utakuwa katika ngazi zote, za kuendesha kampuni yako au ulipo ajiriwa na N.k.

 Unapozungumzia uongozi katika taasisi au kundi fulani la watu. unaongelea muhimili wa hilo kundi, nguvu na maendeleo ya hilo kundi. Kiongozi anatakiwa awe Ana mawazo ya mbele, ya kuendeleza taasisi au kundi, Kiongozi anatakiwa awe ni mtu mwenye maono na malengo ya kesho ya namna gani ya kuipandisha ofisi yake na watu wake kwa pamoja... Kiongozi asiyefaa ni yule ambaye amekaa katika nafasi hiyo huku hajui hata lengo la kampuni au nini anatakiwa kufanya. Kiongozi anatakiwa awe na Busara na awe na ujuzi wa kile anachokifanya ili aweze kubuni vitu vingi zaidi vitakavyo wawezesha kama kampuni iweze kusonga mbele...

Leo hii MeTl group linasonga mbele na kukua zaidi afrika kwa sababu kiongozi wao ambae ni mo dewji ana mawazo chanya na ujuzi wa kile anachokifanya na anatumia ujuzi wake kusoma mazingira na Kujua ni wapi anatakiwa kuwekeza, ni ipi njia sahihi na nyepesi ya yeye kuwekeza sehem akapata pesa zaidi. Ukiwa kiongozi ambaye huna Vision ni ngumu sana kwa kampuni, biashara au taasisi yako kupata maendeleo zaidi na mazuri kwa sababu hakutakuwa na mipango mizuri ya baadae na hivyo kuonekana hamna maendeleo kumbe ni aina ya uongozi mlionao...

UONGOZI HUANZIA NYUMBANI
Mimi nashauri si lazima uwe kiongozi hasa wa kampuni yako kama unajijua huna Vision, huna Mission, huna goals ni bora ukawaachia wenye nayo we ukabakia kusimamia maendeleo yanayopatikana katika uongozi huo. Kuna msemo napenda nihitimishe nao kuwa. Kundi la simba linaloongozwa na Kondoo linaweza kupigwa na Kundi la kondoo linaloongozwa na simba.

Huu msemo una akisi sehemu kubwa sana lakini baadhi hawatauelewa mapema.. ni hivi. Mkiwa na kiongzoi shupavu, mahiri, mwenye uelewa na asiye na uoga mtakuwa na nguvu sana kuliko kuwa na watu mahiri na wenye nguvu wakiongozwa na mtu ambaye hana ujasiri, ujuzi na muoga.

Ndio hilo hapo juu. kundi la simba linaloongozwa na kondoo litakimbia baada ya kiongozi wao kukimbia pale tu amuonapo simba na kundi la kondoo litakuwa limeshinda, na uongozi huanzia nyumbani na sio ofisini tu..

KIONGOZI NDIO DIRA YA KUNDI, TAASISI AU KAMPUNI YA BIASHARA FULANI.

karibu shafiinad na share makala hii ili wengi waweze kusoma zaidi.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here