ALIWEZA KUVUNA ZAIDI YA LAKI SABA KWA MWEZI KWA KUFUNDISHA. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 3 July 2017

ALIWEZA KUVUNA ZAIDI YA LAKI SABA KWA MWEZI KWA KUFUNDISHA.

Leo ninawaletea story ya mmoja wa watu wangu wasomaji wa shafiinad.com ambaye aliniomba ushauri nini afanye juu ya maisha yake baada ya kumaliza chuo na kukaa mtaani bila kupata ajira na huku akiwa hana kitu mtaani, amemaliza shule na anajiona bado tegemezi mpaka wakati huo...

Basi nikamuuliza umesoma nini? akanijibu amesomea UALIMU wa sekondari sayansi na ana mwaka yupo mtaani hajui nini muafaka wake...

Swali la pili nikamuuliza Unakaa wapi na kuna shule ya sekondari...?
Akajibu anakaa Dung'unyi na kuna shule ya serikali na ya private.
na shule hizo zina kidato cha kwanza hadi cha nne.

Basi nikamuuliza tena, umesomea masomo gani na unaujuzi zaidi na lipi..?
Akajibu Physics na Biology.

Kwa maswali hayo nikamalizia na Je kuna Tuition mahali hapo...?
Jibu ni hapana hakuna tuition na ni ngumu kufanya tuition mahala pale..

Ni kwanini ni pagumu kufanya tuition mahala hapo...?
Akasema wazazi wa maeneo hayo ya shule zilipo hawana mwanga wa elimu kwa hiyo hawapeleki sana watoto wao masomo ya ziada wakiogopa gharama ya kusomesha ambayo ni Kila topic ni 3000/= au kwa mwez huwa wanaambiwa 20000/=..

Basi kwa upeo wangu wa haraka haraka tu bila kupoteza muda nikamshauri kuwa nenda kwenu, kaanzishe tuition center, weka gharama ya 1000/= kila topic na jitahidi topic iwe inaisha kwa siku tatu kwa maana topic ya form one mpaka form 4 unao uwezo wa kumaliza ndani ya siku tatu au nne na hapo tukichukulia kwa haraka tu kuwa una wanafunzi 70 total ya madarasa yote na hao 70 kila baada ya siku tatu hadi nne unapata 70,000/= maana yake kwa mwezi unaweza pata mpaka 490,000/=. hii ni kama atafundisha kila siku ila kama ataacha weekend maana yake ana siku nane za kutoa katika mwezi maana yake ana 140,000/= atakuwa ameacha kila mwezi ipotee kirahisi..

Basi jamaa alinielewa akaenda kufungua kituo cha masomo ya ziada na baada ya kuweka hiyo bei ya 1000 alijikuta akipata karibu nusu ya kila darasa katika ile shule ya serikali na kujikuta akitakiwa kuweka mpaka shift ili aweze kuendana na ukubwa wa darasa alilonalo na kujikuta kila baada ya siku tano anapata 150,000/= maana yake katika mwezi kuna siku tano (6) sita ambapo atakuwa anapata laki tisa yaani laki na nusu mara sita.
Lakini yeye kila weekend alikuwa anaenda jmosi tu na juma pili ndio ilikuwa mapumziko maana yake anakosa siku nne katika mwezi kufundisha na hii inamfamya akose lakin moja na nusu tu.

Kwa maana hiyo tukitoa pesa ya jumla ya kwa mwezi alikuwa anapata laki saba na point na hii ni kwa mwezi mmoja tu.

Je ni vip kama ataongeza nguvu kazi ya vijana wenzake wakajikita zaidi katika kutoa mafunzo haya ya masomo tofauti tofauti kwa muda ukizingatia yeye hapo alijikita na somo moja tu la biology.

Vipi kama atafundisha masomo yote mawili...? Angepata mara mbili ya pesa alopata kwa mwezi...

Je unadhani ni kwanini mwanzo wazazi walikuwa hawapeleki watoto wao masomo ya ziada...?

ni kwa sababu bei zilikuwa kubwa na watu walikuwa wanaenda wachache na wenye uelewa wa hali ya juu kwa mwezi... hii inawashinda watu wengi sana katika biashara, utakuta mtu anataka faida ya 1000 na kujikuta akipata watu wachache kulinganisha na yule aloweka faida ya 500 anapata faida kubwa kwa vile wengi wataenda kwake...

na hapo nilitumia slogan hiyo hiyo kumshauri akafanye tuition kwa 1000 kwa kujua wazazi wengi wanaweza kumudu gharama hizi na kupeleka watoto wao kwa wingi katika hayo masomo.

Nadhani hapa kwa story hii wengi wetu tutakuwa tumepata kitu fulani kitakacho tusaidia katika maisha yetu ya mbeleni.

Share na wengine waweze kusoma na kupata mwanga katika hili...

Usiamini kuwa ulichosomea hakina UJASIRIAMALI ndani yake....
Unachotakiwa ni kuwa mbunifu, mpambanaji na Muamuaji wa kutenda kile unachohisi kinaweza kukufanya mtu wa tofauti.

"KUWA WEWE, PAMBANA WEWE KAMA WEWE, USISIKILIZE NINI WATU BAKI WANASEMA."

By Shafii Said Rajabu

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here