JE, UNAJUA LOLOTE KUHUSU HISA? BASI HAPA TUJIKUMBUSHE - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 10 July 2017

JE, UNAJUA LOLOTE KUHUSU HISA? BASI HAPA TUJIKUMBUSHE


Ni kipindi muhimu kujua kuhusu hisa. ingawa pia hapo nyuma niliwahi andika makala kuhusu Hisa, Hatifungani na Gawio na Hivi karibuni utakuwa umesikia makampuni mbalimbali hasa yale ya simu yakiwatangazia watu kununua hisa. Ni muhimu kwako kujua kuhusu biashara hii. Huenda ikawa ya faida kwako au eneo zuri kwako kwa kuwekeza.

SOMA MAANA YA HISA,HATIFUNGANI NA GAWIO HAPA

Mapema niseme kuwa usiogope wala usiwe mwenye hofu. Biashara ya hisa ni ya watu wote tajiri au maskini. Laki moja, laki mbili nk. unaweza kununua hisa. Ili umiliki hisa kwenye kampuni ya simu si lazima umiliki mamilioni kama unavyodhani. Na hapa ndipo tunapokosea na kuwaacha matajiri watambe nasi tubaki kulalamika.

1. HISA NI NINI?
Hisa ni mali kama zilivyo mali nyingine unazomiliki. Tofauti ya hisa na mali nyingine ulizonazo kama shamba, gari, nyumba nk.ni kuwa mali nyingine huweza kushikika au kuonekana kwa macho wakati hisa ni mali isiyoonekana kwa macho. Yumkini zote ni mali tu.
Hisa ni maslahi au haki fulani unayokuwa nayo katika taasisi au kampuni fulani. Ndiyo maana ni mali isiyoonekana kwasababu huwezi kuona maslahi au haki kwa macho.

2. KUMILIKI HISA KATIKA KAMPUNI.
Kampuni yoyote unayoiona huwa inao wanahisa. Wanahisa ndio wamiliki wa kampuni. Kwahiyo hata wewe ukinunua hisa kwenye kampuni yoyote na wewe unakuwa mmoja wa wamiliki.
Haijalishi ukubwa wa kampuni na kiwango chako cha hisa ulichonunua bali ni kuwa ukishanunua tu hapohapo na wewe unakuwa mmoja wa wamiliki. Hata hisa za laki moja nazo zinakufanya kuwa mmoja wa wamiliki.


Kiwango cha hisa zako ndicho kiwango cha umiliki wako. Kampuni ikiwa na hisa 100,000 na wewe ukamiliki hisa 50,000 basi wewe unaimiliki nusu ya kampuni. Ukimiliki hisa 25,000 basi wewe unamiliki robo ya kampuni. Halikadhalika ukimiliki hisa 500, 100, 50, 10, 5 au hata hisa 3 basi hichohicho kiwango chako cha hisa ulichonunua ndicho kiwango chako cha umiliki wa kampuni husika.
Kwahiyo ukinunua hisa 100 Vodacom basi wewe utaimiliki Vodacom kwa kiwango cha hisa hizo ulizonunua. Isipokuwa ni muhimu kujua kuwa anayemiliki hisa nyingi kuliko wote ndiye hujulikana kama mmiliki mkuu wa kampuni.

3. JE, UTAFAIDIKAJE NA HISA?
Kila mwanahisa hupata gawio la faida pale kampuni inapotangaza faida. Kampuni hutangaza faida kila baada ya mwaka au nusu mwaka au vinginevyo.
Utapata mgao kwa asilimia kutokana na kiwango chako cha hisa ulizonazo. Ukiwa na hisa nyingi utapata mgao mkubwa, ukiwa na hisa kidogo utapata mgao mdogo na vivyo hivyo. lakini pia kama kampuni itakuwa imepata hasara na wewe utakuwa umepata hasara, hapa ndipo kuna tofauti kati ya hisa, vipande na gawio.

SOMA HAPA NAMNA UTAKAVYOPATA GAWIO LAKO

4. HISA HUPATIKANA VIPI?
Kampuni husika hutangaza kuuza hisa zake pamoja na bei ya kila hisa. Bei ya hisa moja inaweza kuwa Tshs 1,000/=, 10,000/= nk. Lakini pia kampuni nyingi huweka kima cha chini cha hisa unazotakiwa kununua, mfano kampuni itasema tunauza hisa kuanzia hisa 100 au 50 na si chini ya hapo nk.
Kwahiyo wewe utafuata sharti hilo na mengine yatakayokuwa yamewekwa na utanunua hisa unazotaka.

 SOMA HAPA MAANA YA DHAMANA KWENYE SOKO LA HISA

5. JE, UKINUNUA HISA UNAPEWA NINI?
Ukinunua hisa unapewa cheti cha umiliki wa hisa. Cheti cha umiliki wa hisa ndicho ushahidi kuwa wewe unamiliki hisa katika kampuni fulani. Cheti hicho kama hisa zote ulizochukua umezilipia vizuri na hudaiwi unaweza kukitumia kukopea hela katika mabenki, kama dhamana mahakamani nk.
Cheti cha umiliki wa hisa ni sawa ni sawa na hati ya nyumba/kiwanja, au kadi ya gari na vyombo vingine. Hati hizi zinavyoweza kutumika ndivyo na cheti cha umilki wa hisa kinavyoweza kutumika.

6. JE UNAWEZA KUUZA HISA BAADA YA KUNUNUA.
Ndio, hisa ni bidhaa kama bidhaa nyingine. Unaweza kununua hisa leo na kesho ukiwa na shida ya hela ukauza. Katika makampuni ya umma ( PLC) kama haya ya simu unaruhusiwa kumuuzia yeyote utakayemuona amefika bei.

Ni kiasi gani uuze hakuna anayekupangia. Ni biashara kama biashara nyingine yoyote. Unaweza kuwa umenunua hisa kwa tshs 1,000,000/= lakini ukauza hata 5,000,000/=. Ni wewe tu na mteja wako. Na unaruhusiwa hata kumtumia dalali kukutafutia mteja.
Lakini pia unaweza kuamua kuuza baadhi ukamaliza shida yako na ukabakiza baadhi. Si lazima kuuza zote.
Hayo ni kwa uchache tu kuhusu hisa.

SOMA HAPA TOFAUTI YA DALALI NA MCHUUZI KWENYE SOKO LA HISA

IMEANDIKWA NA Bashir Yakub

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here