USIACHE KABLA HUJAANZA KUFANYA. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 27 June 2017

USIACHE KABLA HUJAANZA KUFANYA.katika kazi zetu hapa Shafiinad.com, tunaongelea kuhusu watu wa aina tofauti tofauti kuhusu kuwa na uwezo wa ku control maisha ya kichumi na kibiashara.
Tunasikia maneno mengi ya visababu, mfano “sina muda”, “niko busy sana”, “sina uwezo au ujuzi mzuri” au pia utasikia “sina pesa”.

Kwa upande mwingine watu wenye sababu zao ni wale ambao wanaonesha wanania ya kufanya jambo, wanasoma sana vitabu, wanahudhuria semina tofauti tofauti, wanafanya tafiti zao za juu ya jambo Fulani, ila kamwe hawajawahi kuthubutu kuanza, kuchukua hatua ya kwanza ya kuanzisha jambo lake. Kwa maana hiyo hawa pia ni wale ambao wanaonesha au wanaweka ugumu kwa kila jambo. Hawaendi kokote, wao wapo hapo hapo.
 
Sio kitu kibaya kujifunza mwenyewe, sio mbaya kuchukua muda wako kufanya tafiti kujua matokeo yako ya baadae ya biashara yako.
Ila hakikisha huachi au kujificha katika tafiti zako za biashara, yaani usione uvivu kufanyia tafiti hata vitu vidogo vidogo. Na kamwe hautajua kila kitu kabla ya kuanza jambo.

Kumbuka, njia nzuri ya kujifunza namna ya kuanzisha na kuendeleza biashara ni kurukia hicho kitu na kukianza. Kwa hiyo katika hatua Fulani za maandalizi yako ni vyema uwe unasema “ni muda muafaka sasa”.

Watu wengi wanasema wataanzisha biashara zao ila kwanza wanataka kuandika business plan, au wamalize mafunzo ya degree ya pili ya biashara, au wajifunze vitu wasivyo vijua juu ya ujasiriamali, lakini miaka mitano baadae bado wanaandikaa tu plani ya biashara au wanasema wanataka kwenda kujiendeleza kielimu.
 
Kwa ajili ya lengo zuri, usiogope sana kuanza biashara. Unatakiwa kujitolea na kuanza kufanya vitu ili ujikute umevifanya. “KUTHUBUTU NDIO KUFANYA”.
Kuna msemo unasema “Fanya kile unachopenda na pesa itakufuata” hii inaweza kuwa kweli ila kuna kitu wamekiruka ambacho naamini kilitakiwa kiwekwe ni “kama utafanya kazi kwa bidii”, maana kusema tu ukifanya kitu ukipendacho haitoshi.
Unatakiwa upambane, unatakiwa uuze kwa bidii bidhaa zako, unatakiwa ufanye kazi kwa bidii zote kuliko mwingine.
Vinginevyo, wote tungeishia kuwa mamilionea tunakula ice cream na kuangalia Tv.

Kuna kitu watu wanaita incubation, yaani muda ambao utachukua mpaka kufikia kuziona pesa katika kile unachokifanya. Ila unachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii na kuamini ipo siku utaona matunda yake. Hapa muongozo ni MATUMAINI na JUHUDI mpaka siku ya mwisho.
Mjasiriamali anatakiwa kuwa na malengo na matumaini kwa sababu njia ya mafanikio siku zote ni ndefu. Mafanikio siku zote huchukua miongo kadhaa kuja kuyafikia yale uliyo yakusudia.

Kuna stori nilisoma ya kampuni ya Rich Dad, Poor Dad ya Robert Kiyosaki ilianzishwa na kuchukua miaka 20 mpaka kuja kuona mafanikio yake aliyojiwekea ambapo kama angejua mapema kuwa itachukua miaka 20, kwanza wasingekuwa na nguvu nayo lakini pia huenda wasingeendelea nayo na kuacha wazo life. Lakini wamekutana na changamoto nyingi sana ambazo zimewakomaza kibiashara na mpaka sasa ni kampuni kubwa na inajulikana sana Duniani na wameweza kubadili maisha yao na ya wengine pia.
 
Kwa hiyo hata wewe amini mafanikio yanaweza kuja kweli kwako wewe, kunaweza kuwa na milima ya changamoto mbeleni lakini utatakiwa kuzishinda ili uweze kufikia malengo yako, mafanikio yako.
Kitu pekee naweza kukuahidi ni kuwa Kama utaweka juhudi, kama hutopoteza matumaini na Juhudi, utaweza kuona mafanikio mazuri ya jambo lako ulifanyalo.
Mtangulize Mungu wako kwa kila jambo na jifunze zaidi kwa kila jambo unalotaka kulifanya.

Share na wengine baada ya kusoma ili na sisi watanzania tuweze kupata mwanga na motisha juu ya kujiajiri na kuwa na maendeleo binafsi na familia zetu.

DUNIA HAITOKUBALI KITU UNACHOKIFANYA MARA MIA MPAKA UTAKAPOFANIKIWA

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here