TUJITUNZE VIJANA,SAFARI BADO ALFAJIRI - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 16 June 2017

TUJITUNZE VIJANA,SAFARI BADO ALFAJIRI


 Shekhe Karume Amri Abedi katika shairi lake la "mzigo nimelemewa" alipata kuandika hivi "mabaya ni machukivu,magumu kuvumiliwa" (beti ya kwanza mstari wa tatu).

Kila ninaposoma shairi hili hua napata tabu sana kujiuliza baadhi ya maswali kutokana na ujana tulionao. Najiuliza kama alfajiri ya safari yetu tumeanza vioja namna hii vipi tutafika alasiri? Je tumesahau kuwa shaba huwa ngumu kusafishika pindi iingiapo kutu? Je tunataraji kubadilika lini kama sehemu muhimu ya kujibadili tunaitumia vibaya?

Labda niseme kuwa hatujawahi kufikiri kuwa siku tutakaypatwa na mauti, picha zetu katika mitandao ya kijamii zitatumika hasa kama utambulisho kwa wasiotujua ama walotusahau? Je utaombewa dua gani kama nyingi ya picha zako ulianika nje maungo yako? Tumewahi kujiuliza kuwa kuna siku tutakuwa katika ndoa zetu? Tumewahi kujiuliza kuwa kila tunachofanya kinapima utu, hekima, busara na maono yetu? ndio hata haya tunayoyaandika katika kurasa zetu hutupambanua kujulikana kuwa sisi ni watu wa namna gani?

Ni vizur tukikumbuka kuwa katika umri wa miaka 15 mpaka miaka 25 ni umri ambao hisia za mwili (body feelings and emotion) hutawala sana katika kuungoza mwili badala ya akili (body mindset) na hicho ndo hupelekea mambo ambayo hutufanya tujutie pindi tunapofikia rika la umri wa miaka 30 na kuendelea.

 Ni vizuri kujua kuwa maisha ya familia zetu (watoto, mke au mume) hutegemea mafunzo na malezi kabla ya kuanza kuzijenga. vijana wa kiume vyema kujua kuwa ukitaka upendeze uhesabiwe ni mume na kwa wanawake ukitaka upendeze na usitirike uhesabiwe ni mke

Ahsanteni, ni mimi New Saidi Msangi nisiyejua mengi katika wanaojua

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here