NAMNA AMBAVYO MJASIRIAMALI ANAWEZA KUKUZA MTAJI WAKE - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 7 June 2017

NAMNA AMBAVYO MJASIRIAMALI ANAWEZA KUKUZA MTAJI WAKE


Wajasiriamali wanapaswa waelewe kwamba kuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza mtaji katika
biashara wanazofanya. Muhimu zaidi ni kufahamu njia hizi ili kuweza kuangalia ni ipi kwa hatua
uliyofikia inaweza kukusaidia zaidi badala ya kukuumiza.
Yafaa pia kujiuliza je ni sababu zipi zinazopelekea wewe kuwa na hitaji la ongezeko la mtaji katika
biashara yako ni nini na matokeo tarajiwa. Kujiuliza maswali haya na mengine itakusaidia kufanya uamuzi
sahihi. Zifuatazo ni njia za kuongeza mitaji ya biashara yako.

JIWEKEE AKIBA

Unapaswa kutenga kwa makusudi sehemu ya faida unayoipata au kipato chako kwaajili ya kukuza mtaji wa biashara yako. Kama utaamua kujenga nidhamu ya fedha kwa kuwa na matumizi yenye kufaa na kujiwekea
akiba mafanikio yatakuja kwenye njia yako.
Iwe kwa mjasiriamali mwenye biashara mpya au inayoendelea ni muhimu sana kufikiria kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara. Uwekaji wa akiba ni moja ya njia ya kukuza mtaji ambayo
haina gharama wala matatizo kuliko nyingine yoyote.
Uwekaji wa akiba ni njia inayoonekana ngumu kati ya watu kwasababu ni njia ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu. Unapotaka kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara au kuendeleza biashara unahitaji nidhamu katika matumizi ya fedha zako.
Jiulize je matumizi ya fedha zako yakoje? Ni yapi yamekuwa matumizi ya msingi na yapi si ya msingi, kwanini usipunguze au kuacha matumizi yasio ya msingi na kuweka akiba ili kuweza kukuza mtaji kwaajili ya biashara yako.
Jiulize unatumia kiasi gani cha fedha zako kwaajili ya ‘vocha’, unatumia kiasi gani kwaajili ya pombe, unatumia kiasi gani kwaajili ya starehe, vipi michango ya harusi, je unatumia kiasi gani kwaajili ya burudani nyingine ambazo si za msingi!
Kaa chini na utafakari juu ya mapato na matumizi yako na angalia ni kwa namna gani unaweza
kuweka sehemu ya mapato yako kama akiba kwaajili ya aidha kukuza mtaji wa biashara unayofanya au kuanzisha biashara mpya na malengo mengine ya baadae.

INGIA UBIA

Njia nyingine ya kuweza kukuza mtaji wa biashara ni kuingia ubia (partnership). Kuingia ubia ni njia
inayowakutaniasha watu ambao mahitaji yao yanafana ila pande mmoja unaweza ukawa una hili
na mwingine umekosa hili hivyo inabidi kuungana.
Kwa mafano kama wewe una mali X na umekosa mali Y ili kuweza kufanya jambo fulani basi unaweza kuingia ubia na mtu mwenye mali Y ili kila mmoja aweze kufikia malengo yake husika. Makampuni yanaingia ubia itakuwaje kwa nyinyi wajasiriamali!
Pamoja na njia ya ubia kama namna ya kukuza mtaji wa biashara, jambo hili limekuwa gumu kwa watu wengi kwani badala ya kutumia njia hii kujijengea maendeleo wabia wengi wamejikuta wameingia kwenye ‘bifu’ zisizo na msingi na hatimaye kushindwa.

IKIBIDI OMBA MKOPO

Ikibidi omba mkopo, nasisitiza kama italazimu basi tumia njia hii kukuza mtaji wako wa biashara. Hii
ni njia kubwa zaidi inayotumiwa na wajasiriamali ni njia ambayo inahusisha gharama na ambayo
imewaacha baadhi ya wajasiriamali katika matatizo.
Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitumia Benki, SACCOS, VICOBA na taasisi nyingine za mikopo
midogo (Microfinance Institutions) kutafuta fedha ili kuweza kukuza mitaji ya biashara zao. Nashauri, mikopo si ya kukimbilia yafaa kujiuliza kwanza.
Kuepuka matatizo ya kukuza mtaji kwa njia ya mikopo toka taasisi mbalimbali za fedha, yafaa mjasiriamali kujiuliza baadhi ya maswali, lengo kuu la kujiuliza maswali haya ni kuweza kujifanyia tathmini kama kweli unahitaji kukuza mtaji kwa njia ya mkopo.

Swali la kwanza jiulize, je una malengo gani na fedha utakazokopa? Je malengo uliyonayo juu ya mkopo unaoomba yana vihatarishi vipi, hii ni kwasababu taasisi nyingi za fedha hupenda kutoa mikopo kwenye shughuli ambazo zina usalama na endelevu.

Swali la pili la kujiuliza, je unahitaji kiasi gani cha fedha ili kuweza kukuza mtaji wa biashara yako ?
Kuna wajasiriamali ambao huenda kukopa lakini hawajui wanahitaji kiasi gani, hawajajipanga !
Wanachojua wanataka kukopa tu, mambo mengine baadae.

Swali la tatu la kujiuliza, ni lini hasa unahitaji mkopo huo ? Wapo ambao wanakopa kwanza halafu baada ya kupata mkopo ndio wanakaa chini kupanga mipango. Kaa chini ujiulize kama kweli unataka mkopo ungependa upate lini huo mkopo na kwanini.

Swali la nne la kujiuliza ni, je utahitaji mkopo huo kwa muda gani ? Kama utahitaji mkopo kwa muda
mfupi na kwasababu zinazoeleweka, itakuwa rahisi kwako kushawishi taasisi ya fedha kukupatia mkopo badala ya kukaa bila kujua muda wa hitaji lako.

Swali la tano na la msingi ni juu ulipwaji wa mkopo, ukiomba mkopo na kupewa je utaulipaje ?
Je una vyanzo gani vya mapato ambavyo unaweza kuvitumia katika kuhakikisha mkopo unarejeshwa
pamoja na gharama zake (riba) kwa muda uliopangwa .

Swali la sita la kujiuliza ni ikiwa mambo yataenda mlama, nini kitafanya mkopo ubaki salama ? Hapa
wakopeshaji wengi huhitaji dhamana za mkopo (collateral) ili kuweza kwa namna moja au nyingine
kuulinda mkopo uliotolewa ili ubaki salama, kulipika!

Ni matumaini yangu ndugu mjasiriamali, katika kutafuta namana bora ya kukuza mtaji wa biashara yako utaangalia ile ambayo inaendana na hali halisi uliyonayo badala ya kukurupuka na kufuata mkumbo, kwa njia hii utaweza kuepuka matatizo yasiyo lazima.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here