Bill Gates Wanaofuata kutokea Africa. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 18 June 2017

Bill Gates Wanaofuata kutokea Africa.
Leo nimependa nitoe hadithi au story ya watu flani hivi ambayo dhamira kuu yangu ni kuwonesha watu ni namna gani tunaweza kufanikiwa kama tutaweza kujua na kutumia fursa zinazotunguka, kama ujuavyo fursa ni shida iliyokuzunguka wewe, basi na hata mafanikio yapo pia yamekuzunguka, sasa ili uwe kama bill gate ni kazi inayohitaji kujidhatiti zaidi katika kile unachofanya, twende pamoja.

Anesi (Miaka 17) na kaka yake Osine (miaka 14), ni vijana wawili wa mfano wa kuigwa kutokea Nigeria..

Walipokuwa na umri wa miaka 9 na 7, wote wawili walianzisha biashara yao iliyooitwa "BluDoors"(http://www.bludoors.com/), Walikuwa inspired sana kutumia jina  "Doors" kutoka kwenye jina Bill Gates' ambalo analitumia mwenyewe kama jina la bidhaa yake ya,"Windows".

Story ya hawa jamaa, ni story nilioona leo hii tushirkishane kwa sababu ina mwanganza wa ni namna gani ujasiriamali unaanzishwa. katika muongozo wa  "Fast Follower", kwa kuangazia sana juu ya hawa jamaa, nimejifunza kuwa, mfano, katika huduma au bidhaa ambazo zina kuumiza kichwa wakati wa kuzitumia, hutakiwi kukaa na kulaumu wengine lakini  badala ya kulaumu maduka madogo madogo, au watengenezaji, we kaa chini na tengeneza kitu kizuri na kikubwa zaidi ya hicho.

Hichi ndicho kilichotokea kwa hawa jamaa wawili:

Ingawa walikuwa katika umri mdogo wa miaka 9 na 7, walikuwa tayari wametengeneza tabia ya kupenda kuchezea computer, na miaka miwili mbeleni, waliamua kujifunza CODING(lugha ya computer). Kuna jamaa mmoja aliwahi sema mabilionea wajao wa Africa wengi watatokea katika wale waliojifunza lugha ya computer. Huko China, Coding sasa ndio imekuwa deal na chuoni wanasomea kwa miaka mitano (5)!

Japo Hawa jamaa walijifunza kwa kupitia mitandao iliyopo kwenye internet ambayo ni bure mfano Code Academy.


Sasa baada ya kujiona wako vizuri waliona kuna haja ya kutengeneza browser ambayo itatumiak kwa simu ndogo za smartphone na zile zisizo na viwango vikubwa ila ikawa na kasi na utendaji mzuri wa kazi katika hizo simu ndogo, ambapo hizo simu haziwezi tumia browser zzilizopo sokon sasa hivi, wanapotumia inawaletea matatizo mengi (HAPA WAMEONA FURSA). 

Hebu pata picha hawa vijana wadogo, wamekaa na kuwaza ni namna gani wanaweza kutatua tatizo la browser kwenye simu zao ndogo na zisizo na ubora mkubwa, wakapata na wenyewe kitu kama "Google Chrome".

Na mpaka leo hii wana biashara yao ambayo wanaitangaza ambayo ni browser yao waliyoipa jina la, "Crocodile Browser Lite". Na inapatikana bure kwenye Google Play Store: (https://play.google.com/store/apps/details?id=com.webs.enterprisedoor).

Kwa hiyo kama unataka kuona akina "Bill Gates"wajao, tembelea hiyo browser na wewe pia jipinde ugundue fursa ili uwe ,Mjasiriamali halisi, na hivi Bill Gates na Paul Allen walivyoanza.

Simaanishi au kukuaminisha kuwa unatakiwa ujifunze lugha ya computer ndio ufanikiwe, hapana, niko hapa kukupa mfano wa hawa vijana na namna walivyoweza kugundua fursa na kuifanyia kazi wakiwa bado wapo katika umri mdogo, kwa hiyo wewe hapo ulipo pia unaweza gundua kitu kitakachokuingizia pesa na kukifanya kama miliki yako kama watu wengine.

Wacha nikupe Siri:

Hawa jamaa, hawatakuwa wanatafuta pesa hapo baadae, bali pesa itakuwa inawatafuta wao.
                        "Provision always follows a great VISION" 

Ahsante na nikutakie siku njema na mafanikio mema,
Share na wengine ili na wao wapate kujua na kujifunza juu ya ujasiriamali na maisha kwa ujumla,
Like page yetu ya facebook ambayo inaonekana pembeni au kwa chini baada ya hii post.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here