NINI NI MALENGO YAKO KATIKA UCHUMI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 26 June 2017

NINI NI MALENGO YAKO KATIKA UCHUMI.
Naomba nieleweke kwanza kabla hatujaendelea mbele,: kuwa na biashara yako siko kitu rahisi kama wengi wanavyofikiria. Haimaanishi kuwa ukifanya kazi kwa muda mchache utafanikiwa.
Kutakuwa na changamoto kubwa katika mipangilio yako, ila kama sababu ya wewe kuingia katika biashara ni kwa sababu unafikiria utakuwa na uhuru wa muda, basi unatakiwa ukae chini na ufikirie tena hilo wazo lako.


Ila kwa wale ambao wanataka kuanzisha biashara zao kwa sababu wana ndoto wanayotaka kuifanya iwe kweli, hapo sawaa endelea. Kitu pekee kitakacho kufanya uweze kubakia katika mstari wako ni kufanya kazi kwa muda mwingi naa kuwa na mawazo na njia Sahihi za kufikia malengo yako, uwe na kitu kinachoeleweka katika jamii ili hata mtu akitokea akajumuika nanyi katika hiyo biashara aweze kuelewa na kuhisi kweli kuna kazi iliyopangiliwa inafanyika hapa.
Kwa hiyo kuandaa lengo la biashara, nini mnategemea, ndio point ya kwanza ya kuanzia. Na ndio kitu kitakachokupa nguvu katika vikwazo vyako, na itakuwa ndio mwanga wa baadae wa biashara yako.

Kwa hiyo unatakiwa kuandaa plani ya biashara yako.
Unafanya hii biashara kwa ajili yako tu? Na je kutakuwa na kanuni nyinginezo? Nani ataenda kufanya nini? Nani atakuwa muamuzi wa mwisho?
Ni vizuri ukaiweka safi plani yako ya biashara kadri uwezavyo, lakini usiishie hapa.

Na wala usiwaze kuwa hutaweza kuifanya ipasavyo, kwanza amua kuanza biashara.
Katika point nyingine ni vyema ukatengeneza urafiki na wale waliofanikiwa ili waweze kukuongoza katika mafanikio ya biashara yako.

Kwa hiyo no lazima kila mtu mwenye nia ya kupata mafanikio katika jambo Fulani awe na malengo juu ya lile jambo analotaka kulifanya, hii ndio nguzo ya kwanza ya kuweza kuwa na biashara au jambo lolote la kipekee.
Wanasema unatakiwa uwe na vision then lengo halafu uwe una mipango mikakati ya kufikia lengo.
 
Kwa leo napenda kuishia hapa, lengo letu tukumbushane na kupeana moyo kwa wale wenye nia ya dhati ya kufanikiwa. Tuweze kupata maendeleo tunayo yatamani.
Unaweza ku share hii post ili na wengine waweze kusoma zaidi.

TO DARE IS TO DO.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here