HAKUNA UMRI MDOGO KWENYE KUANZA MAFANIKIO, YOTE YANAWEZEKANA UKIAMUA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 25 June 2017

HAKUNA UMRI MDOGO KWENYE KUANZA MAFANIKIO, YOTE YANAWEZEKANA UKIAMUAKuwa mjasiriamali hakuendani na umri wako, jinsia yako, unapoishi, au umesoma kwa kiasi gani.
Ni juhudi, ugunduzi, nia ya dhati ya kubadili ndoto yako kuwa biashara inayoonekana.
Na pia ujasiriamali ni kuwa na macho ya kuona fursa pale inapotokea. Hichi kipaji hakihitaji umri wala jinsia.
Napenda kuwapa story ambayo nimeisoma ya mtoto mmoja Anaitwa Kim.
Kim ni msichana mwenye umri wa miaka 14 anatokea Florida. Alianza kuweka pesa yake kwa kwenda garage na kuokota vyuma chakavu (skrepa) ambavyo vimetupwa na akawa anavihifadhi katika hema lao.
Kwa muda wa miezi kadhaa aliweza kukusanya vyuma chakavu vya dola $6,000.
Kwanza kabla hatujaendelea, kuna vitu viwili hapa tuvione.
1.Hakuhitaji mtaji ili aweze kutekeleza lile wazo lake (vitu vyote aliviuza kwa wale wale ambao walivitupa)
2.Pia aliweza kubuni chanzo cha mapato yake kwa kutumia Hivyo vitu chakavu.
Kwa haraka haraka kwa umri huo wa miaka 14, unaweza ukadhani angewaza kununua gari. Ila hapana, huyu msichana alianza kutafuta nyumba za kupangisha zinazouzwa, akapata nyumba ambayo ilikuwa na thamani ya dola $16,000, ilikuwa 2012, ambapo nyumba nyingi sana zilikuwa zikiuzwa sana na kwa bei ya chini.
Huyu msichana alikuwa MAKINI, ANAYEFIKIRIA. Akawaza kuwa anaweza akapata kwa bei ya chini kabisa, kwa hiyo akaongea nao na akaweza kufikiana dola $12,000. Lakini pia kwa umri wake ilikuwa ngumu kupata mkopo, kwa hiyo mama ake ikabidi awe mfanyabiashara mwenzake kwa ku share pesa waweze kuinunua hiyo nyumba. Kwa hiyo akaweza kuwa na nyumba yake ya kupangisha akiwa na umri wa miaka 14. Na kwa sasa inasemekana amepata nyumba nyingine.
Kumbuka alikuwa na umri wa miaka 14. 
 
Hii stori nimeandika kwa lengo la kuonesha watu kuwa si lazima tuwe na mtaji mkubwa wa kuanza biashara, ila tunahitaji kuwa wabunifu na watu wa kufatilia fursa.
Baada ya kuipata fursa tuifate na kuihakikisha tunaiweza na kuona mafanikio yake.
Excuse yoyote ya kutokuwekeza pale ulipotakiwa kuwekeza, kwa kutokuchukua uamuzi, na ulitakiwa uchukue uamuzi kwa muda huo, sio nzuri ila bado unao muda. Kwa sababu kama msichana wa miaka 14 ameweza kufanya hili, na wewe pia unaweza. Hakuna haja ya excuse tena.
Karibuni Shafiinad.com muweze kupata motisha, mawazo na ushauri juu ya ujasiriamalia ambao wenzetu wa mataifa yaliyo endelea elimu hii huanza kutolewa mashuleni, na watu wenye mafanikio pia huwapa watu fursa ya kujifunza bure. Pia unaweza kushare zaidi tuweze kupata kusoma zaidi.

YOU ARE NEVER TOO YOUNG TO CHANGE THE WORLD

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here