HAKUNA UZEE KWENYE UJASIRIAMALI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 25 June 2017

HAKUNA UZEE KWENYE UJASIRIAMALI.
Ukianza kujiuliza uliza swali la kuwa umekaribia kuzeeka au kustaafu, hapo utakuwa umechelewa kwa kufikia mafanikio ya ndoto kubwa, kwa kuwa tu huwezi kuchukua risk, leo hapa ntapenda niwape maneno juu ya hii inshu.

Kuna tafiti kadhaa zilizofanywa ambazo zinaonesha watu wenye umri wa kustaafu wanaanzisha kampuni kwa haraka na kwa urahisi kuliko umri wa chini, hasa wale wenye umri wa kuanzia miaka 55-64 ndio nina waongelea hapa.

Baadhi ya watu wanaita phenomenon au grade ya “Silver Startups.” Mi naita hii smart.
Sababu moja wapo ya kuwa hivi ni kuwa watu wengi wanakuja kugundua kuwa kuna meng sana katika maisha kuliko katika kazi.
Labda kustaafu kumewafanya wao wakae na kufikiria upya juu ya ujuzi wao, au wameweza kugundua kuwa, walikuwa na miaka mingi katika dunia na hawataki kupoteza tena ndoto zao mpaka zitimie.
Wanataka kutafuta kitu ambacho kipo katika ubora zaidi na kitawasaidia katika maisha yao.

Nikupe mifano baadhi ya watu ambao hawakuhangaika wakati wa ujana kujiwekezea kibiashara lakini wamekuja kujiwekeza wakati wa uzeeni.?
Momofuku Ando, mzee aliyeamua kuanzisha ramen na kubadili maisha ya wanachuo, na hakuifanya hii mpaka alipofika umri wa miaka 48.
Rodney Dangerfield Hakugundua fursa mpaka alipogundua kuandaa show ya Ed Sullivan akiwa na umri wa miaka 46.
Mzee tunayemjua kama Colonel Sanders alipokuwa na miaka 62 akaanzisha mgahawa wa fast food chicken restaurant chain Kentucky Fried Chicken, ambao ni maarufu sana mpaka sasa.
Henry Ford akiwa na umri wa miaka 45 ndipo alipo tengeneza Model T Ford.
Julia Child hakuchapisha kitabu chake cha kwanza cha mapishi mpaka alipofika miaka 50.
Laura Ingalls hakuchapisha kitabu chake cha kwanza cha mbuga za wanyama mpaka alipofika miaka 65. Mifano ni mingi mingi zaidi, na hao wote ukiwatafuta utawapata google na history zao.
Sasa basi Labda umekamata sana taaluma yako na umegundua kuwa huna muda wala nia ya kustaafu kwa sasa. Lakini jua Umepata ujuzi na uwezo mkubwa wa kupata pesa, na hizo ndizo funguo za mafanikio katika knowledge inayohusu uchumi.

Katika ujasiriamali, Tunahitaji watu wenye kujua ni kwa jinsi gani na wana uzoefu gani katika maisha yao, na maisha ya kibiashara na mara nyingi hao ndio wale watu wenye mvi kichwani ndio huonekana wako bora na wazuri zaidi(wazee wanajua vingi sana).
 
Lakini watu wengi katika umri huu hawaoni kama tuonavyo. Wanawaza kuwa wao sio watu Sahihi au wanajiona ni wazee sana kiasi hawawezi kuwa viongozi wa kutoa mawazo. Hawafikirii kuwa kiongozi (kuongoza). Hii kwa kifupi si kweli.
Kuwa mzee sio sababu ya wewe kutokukimbilia ndoto zako. Kama sio sasa, ni lini sasa utafanya kile unachotakiwa kufanya?
Amini unaweza, Kila kitu kinawezekana, Mtamgulize Mungu wako kwa kila jambo.
Karibu sana Shafiinad na unaweza kushare na wengine ili tusambaze makala hii ya kutiana moyo katika kutafuta mafanikio na unafuu wa maisha yetu.
life begins at the end of your comfort zone.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here