KILIMO CHA BAMIA, NAMNA YA KULIMA MPAKA UVUNAJI - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 2 June 2017

KILIMO CHA BAMIA, NAMNA YA KULIMA MPAKA UVUNAJI


Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.
Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.Jinsi ya kupanda bamia
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kilimo cha bamia.

  1.   Hakikisha unatumia mbegu bora
  2. Panda kwa nafasi
  3. Mwagilia maji ya kutosha kulingana na hali ya hewa
  4. Palilia shamba vizuri
  5. Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati
  6. Vuna kwa wakati unaotakiwa


Jinsi yakupanda
Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.
Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari.
Kwa aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
 
Umwagiliaji
Kama unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika

Palizi
Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia

Wadudu waharibifu
Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri mwekundu.
Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.

Magonjwa
Bamia hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na
ushauri wa wataalamu wa kilimo eneo ulipo.
 
Uvunaji wa bamia
Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
Unashauriwa kutumia kisu kuvunia na uhakikishe unavuna bamia na kikonyo chake ili kupunguza kuharibika kwa bamia
Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
Sijajua kwa sasa bei ya kilo moja inauzwaje sokoni au mafungu kwa hiyo kwa wale wapimaji wanaweza jua utapata faida kiasi gani katika heka moja.

Tembelea zaidi blog yet hii tujifunze kwa pamoja juu ya kilimo, ujasiriamali na kupeana  moyo juu ya kufikia ndoto zetu.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here