USITHUBUTU KUJARIBU KINA CHA MTO KWA KUTUMIA MIGUU YOTE MIWILI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 7 May 2017

USITHUBUTU KUJARIBU KINA CHA MTO KWA KUTUMIA MIGUU YOTE MIWILI.
Habari ndugu msomaji wa makala zetu za hapa shafiinad blog, leo hii napenda tuongelee maendeleo katika nafasi ya kuthubutu ama kujaribu.
Kila siku huwa naandika kuwa ukithubutu ndio umefanya au kujaribu ndio kufanikiwa.
Hapa leo napenda kutoa onyo au ushauri kabla ya watu kuenda kuthubutu kufanya lile wanalowaza kulifanya.

Leo nataka niongelee kwa sababu kuna watu wengi sana nimewaona katika wakati ambao wanajitolea kujaribu wakijaribu wanajikuta wamefeli na inampelekea yeye kuona hawezi fanikiwa.
Hapa leo nataka nikuhakikishie kujaribu ndio kuweza, ila unajaribu vipi.
lazima ujifunze jambo vizuri kabla ya kuanza.

mfani mimi leo hapa naongelea kutokuwekeza pesa yako yote katika kujaribu biashara moja kwa sababu inaweza ikawa na changamoto ambazo hujazitarajia na zikakufanya ushindwe. na madhara yake unajikuta pesa yako yote uliwekeza katika huo mradi, una bakia ukiamini wewe si wakufanikiwa, wewe ndio umeumbiwa uwezo huo huo hakuna uwezo wa ziada ulionao, lakini kwa ukweli ni hapana ila ulikosea kuwekeza mtaji wako wote.

matajiri wakubwa wanasema huwezi kufanikiwa bila kukopa ila mimi nasema huwezi kuanza kukopa bila kujaribu japo kwa kiwango kidogo sana kuhusu hiyo biashara au mradi unaotaka ukaanzishe.
ukisha ujua vizuri ndipo utaweza kopa na kuutanua zaidi huo mradi wako.
lakini utaanzaje ndio hapa lazima uanze kwa kujaribu na kipato chako kidogo na sio chote ili ujue changamoto zake na faida yake na hata soko lake la huo mradi wako.
 

Watu wengi hata mimi nimewahi wekeza katika mradi mmoja wa kilimo na nikajikuta nimeshindwa nikapata funzo la wapi ilipo shida iliyopelekea mimi kushindwa. na nilipoijua niliweza kubadili mfumo wa kuwekeza na sasa naona matunda ya huo mradi lakini kama ningekuwa nimewekeza pesa yote nisingeweza kuwekeza tena katika huo mradi ambao kwa sasa naona mafanikio yake.

Kama una lolote naomba tushirikishane ili tuweze kufikia malengo yetu.
karibu shafiinad.com tujifunze kwa pamoja kuhusu mafanikio na njia za kufikia mafanikio yetu.

AMINI UNAWEZA
ISHI NDOTO YAKO.

like facebook page yetu ya shafii blog ili upate makala nyingi zaidi kwa muda mfupi kila siku.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here