USIRIDHIKE NA KIPATO KIMOJA TU, WEKEZA ZAIDI UONGEZE KIPATO CHAKO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 5 May 2017

USIRIDHIKE NA KIPATO KIMOJA TU, WEKEZA ZAIDI UONGEZE KIPATO CHAKO.Karibu shafiinad blog tuzungumze mambo ya biashara, hapa tuna share mawazo ya biashara na wewe mwenzangu ambaye unapenda biashara na unatamani mafanikio ya hali ya juu.
Mungu yupo atatutimizia tu Ipo siku.

Katika mada yangu ya leo napenda tuongelee katika maswala ya kuongeza kipato chako baada ya kuongelea sana namna ya kupata kipato chako.

Leo napenda nitoe mifano ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza isiwafurahishe baadhi ya watu.

Tunaposema uongeze kipato chako, tuna maana unatakiwa ujiongeze kutoka katika uwezo wa fedha ulionao kwenda juu zaidi.
kutokea kwenye biashara uliyo nayo kwenda biashara nyingine na hata hivyo hivyo mshahara wako kutokea ulipo mpaka ufike juu zaidi ya huo.

Napenda nitoe mfano ambao ni wa kawaida na hauhuisiani na mtu yeyote.
Kuna mfanyabiashara fulani yeye alikuwa anafanya biashara ya vyakula katika eneo fulani na malighafi ya hivyo vyakula alikuwa akivinunua sehemu fulani.

Sasa baada ya muda akagundua kuwa watu wanaofanya bishara kama yake wamekuwa wengi na ilisabababisha faida yake kupungua.
alicho ona na kujifunza ni kuwa anatakiwa aongeze njia ya kupata faida.
swali atapataje faida zaidi...!?


kwa kawaida unaweza waza ni kuacha kufanya hiyo biashara lakini hapana jibu ni rahisi sana ni kuwekeza zaidi katika biashara hiyo kwa njia ya nyuma ya pazia.

bila watu kujua utafanyaje.
Mfanyabiashara huyu jambo aliloona zuri ni kuwa aliona wote wanategemea kwenda nunua malighafi za vyakula wauzavyo kwa mtu mwingine ambaye na yeye anapata faida.

njia ikawa ni kuanzisha mradi wa kuuza malighafi za vyakula hivyo huku akiendelea na bishara yake ya vyakula.

kwa mantiki hiyo atakuwa akipata faida mara mbili atapata faida kama kawida ya kuuza vyakula lakini pia atanunua malighafi dukani kwake na ambapo huko pia atapata faida kupitia mauzo hayo.

kwa maana hiyo mtaji na faida ya huyu mtu unakuwa na utazidi kukua zaidi kadri atakavyo anzisha biashara mpya kila mara.

kwa hiyo wazo langu leo hapa au ushauri wangu hapa ni kuwa kuna haja kubwa ya kuongeza miradi zaidi ya mmoja ili upate faida na kipato cha zaidi..

usitegemee mshahara tu wa kazini maana hautakufanya ufanikiwe zaidi na asilimia kubwa ya wafanyakazi wengi wanakuwa na maisha ya kuweza kula na kusomesha lakini sio ya kuwa huru na pesa yao katika matumizi.

Usiamini sana kuajiriwa amini kujiajiri ndio njia ya haraka na rahisi ya kufanikiwa.

Ajiriwa kupata mtaji lakini usiajiriwe kukufanya upate mafanikio makubwa.

Karibu shafiinad.com ujifunze zaidi mambo ambayo yanaweza kutupa nafuu na mwanga wa kuwa na maisha yenye mafanikio.

believe you can.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here