USIHIFADHI KILE KILICHOBAKIA BAADA YA KUTUMIA, ILA TUMIA KILE KILICHOBAKIA BAADA YA KUHIFADHI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 7 May 2017

USIHIFADHI KILE KILICHOBAKIA BAADA YA KUTUMIA, ILA TUMIA KILE KILICHOBAKIA BAADA YA KUHIFADHI.
Habari Ndugu yangu msomaji wa makala zangu kupitia blog ya shafiinad. leo hii napenda tuongee pamoja kwa kifupi nini unachotakiwa kufanya katika maisha yako ya sasa na kwa ajili ya maisha yako ya baadae. Tumesoma mambo mengi sana kupitia blog hii na leo hii napenda tuongelee kuhusu kuhifadhi pesa,

Kuna njia nyingi sana ya kuhifadhi pesa na moja ya njia ya kuhifadhi pesa ni kuweka bank, sasa leo tuongelee mfano wa kuweka bank tu, ingawa kuna makala nimewaelekeza juu ya hasara ya kuweka pesa bank kama ndio bado mfanyabiahara mdogo.

Watu tunaweka pesa kwa njia nyingi na mfano wa bank ni rahisi, tuchukulie unapata fedha iwe mshahara au faida katika biashara, unapata 500,000/= laki tano.
Kwa kawaida tunasema unatakiwa uhifadhi kile ulichokipata na baadae unatumia ulichobakisha.
hapa kwa kufata huo msemo ambao ndio mzuri unaweza kadiria kila mwezi kuweka laki tatu 300,000/= na laki mbili kujibana katika matumizi mengine.

faida ya hii ni kuwa utajituma zaidi kuweza kuziba mapengo yatakayotokana na kuweka pesa yote uliyoipata katika bank.
na kadri unavyojituma ndipo kipato chako kinaongezeka na unajikuta unazidi kupata pesa zaidi ya kuweka na kutatua shida na matumizi ya nyumbani.

 
Hii ni faida kubwa sana maana utajikuta umeanzisha mradi ambao utakuingizia zaidi kuliko ulipo sasa.
lakini kama utafata mfumo wa kuweka kile kilichobakia baada ya kutumia maana yake utakuwa na saving ndogo na utakuwa hupati hamasa au changamoto itakayokufanya ubuni na utafute njia nyingine ya kupata pesa maana utakuwa huna shida na hukai ukawaza kuwa kuna kitu kinakudai kw vile umeshatumia.

pia hasara nyingine ni kuwa hutaweza kuweka pesa ya kutosha na siku nyingine utaweza kupitiliza kabisa bila kuweka hicho kidogo unachotaka kuweka kwa kujikuta pesa yote imeisha baada ya matumizi.

Jiwekeze upate faida zaidi.

Jitume na kila siku kuwa mbunifu wa mambo ili uweze kujiongezea kipato chako na kumbuka bila wewe kuamua huwezi fanikiwa na siku zote ili ufanikiwe unatakiwa ujue kilichomo ndani yako.

Be yourself, Work hard, learn everyday kupitia shafiinad.com blog inayotoa mafunzo bure ya kupeana moyo na motisha.

Imeandikwa na Shafii Saidi.
MLS

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here