USIWEKE MAYAI YOTE KATIKA TRAY MOJA, KATIKA UWEKEZAJI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 7 May 2017

USIWEKE MAYAI YOTE KATIKA TRAY MOJA, KATIKA UWEKEZAJI.


Leo napenda tuongelee mada hii ya uwekezaji, Ambapo natamani sana nieleweke kwa hili ninaloamini lina manufaa zaidi kwetu sisi ambao ni vijana au wa Tanzania wenye uchu wa maendeleo yetu na ya nchi yetu pia.

Katika uwekezaji kila mtu anayewekeza anatamani sana awekeze na apate faida kibwa zaidi ya hiyo aliyonayo na ili ufanikishe hilo ni vizuri ukatumia hii kanuni ya kutokuweka mayai yote kwenye tray moja.

Mfano tuchukulie una milioni kumi na unataka uwekeze katika biashara fulani, biashara hiyo mfano kwa mwezi inakuingizia milioni moja kam faida.
Hii ni pesa kubwa na nzuri sana kwa mtaji wa milioni kumi, lakini kwa kufuata kanuni hii mi mwenyewe naamini utapata faida zaidi ya milioni moja kwa kufanya hivi.

umachukua ile milliono kumi unaigawanya katika makundi ya milioni moja moja au mbili mbili lengo ni kupata biashara nyingi zaidi ya moja ambazo kila moja itakuingizia kipato chake, na amini kuna siku biashara moja haitakuwa nzuri lakini nyingine itakuwa nzuri na hapo utapata faida zaidi ya milioni moja wakati huo ile moja siku kukiwa hakuna biashara, basi biashara yako itasimama kwa siku hiyo na utakuwa huna chanzo kingine cha kuingiza kwa siku hiyo, ila pia kadri mitaji midogo inavyojilipa ndivyo inavyo ongezeka kukua na kukupa faida nyingi zaidi ya kuwa na biashara moja tu.

Wazo hili nimeliona katika wafanya biashara wakubwa kama akina Mo dewji, Bakhresa na wengine.

wao wamegawanya biashara zao katika kila kona ya aina ya biashara wakiamini leo usipokunywa juisi zao basi utakula unga wao, kama si unga basi utatumia kibiriti chao tu.
kwa hiyo hii inamfanya apate faida kila siku kuliko wangekuwa na biashara ya juisi tu. ambapo siku ukisema hunywi na wao watakuwa hawajaingiza faida.

Kwa mfano huu mdogo nliotoa nadhani mnaweza kuwa mmepata picha halisi ya nini naongelea hapa na shafiinad tunajifunza vitu kila siku ili tuweze kupeana mawazo humu ndani tuweze fikia malengo yetu kwa pamoja.

Amini unaweza.
ishi ndoto yako.

Kuthubutu ndio kuweza.

Karibu na wasambazie wengine link hii wapate kujifunza zaidi.

Like facebook page yetu ya shafii blog.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here