TABIA ZA WATU WENYE MAFANIKIO, HUWA WANAONGELEA FURSA ZA MAENDELEO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 22 May 2017

TABIA ZA WATU WENYE MAFANIKIO, HUWA WANAONGELEA FURSA ZA MAENDELEO.Habari za Muda huu, na wakati huu ndugu yangu msomaji, mjasiriamali mwenzangu na pia mwanamaendeleo, leo hapa nataka kuongelea jambo sio jipya lakini lina manufaa zaidi.

Siku zote watu wenye mafanikio na wale wenye chachu ya mafanikio hupenda kuongelea maswala ya fursa, nafasi za kuweza kuwatoa kimaisha au kuwaendeleza zaidi katika mafanikio yao. na wanatumia muda mwingi sana kupeana habari hizo kwa sababu ni watu wenye chachu ya mafanikio.

Wanaamini kuwa bila kubuni na kupata njia mpya ya kufanikiwa kila siku, hawataweza endelea pale walipo na wanaweza pia kurudi chini badala ya kupanda juu kwa vile hawakuziona fursa..

Lakini watu wasio na mafanikio makubwa katika maisha yao au watu ambao hawajafanikiwa mara nyingi hawana muda wa kupiga story za fursa bali huwa wana muda wa kupiga story nyingine za kuchekesha, Kuwapa habari ambazo hazina umuhimu kwao na pia hukaa kujadili watu na kujikatisha tamaa ya kuweza kufanikiwa hata baada ya mtu mmoja wapo akitoa wazo la fursa ili muweze kufanikiwa kimaisha..

Kwa hiyo kwanini ukae na watu wa namna hii, kwanini ukae bila kujipa jambo jipya kila siku lenye maendeleo na maisha yako?
kwanini unapenda kushinda vijiweni na watu ambao hawana malengo na mipango ya kesho yao..?

Wakimbie, jitenge nao, tafuta watu wenye mafanikio wawe ndio walimu wako, roll model wako na wafanye kuwa chachu ya mafanikio yako,?

kwanini Uamini kuwa wewe ni masikini, kwanini unajidhoofisha nafsi kwa kujikatisha tamaa katika mafanikio yako,?

Amka sasa, Achana na vijiwe visivyojenga, changamkia fursa, jifunze vitu vipya kila siku ambavyo vitakufanya uumize kichwa mara kaa mara na vitakupeleka mbali kimafanikio ya maisha yako...

Usiwe mtu wa kulaumu unapokosea au mtu anapokosea ila jipe au mpe moyo wa mafanikio ili tufike mbali wote..

shafiinad.com tunaamini kabisa kuwa mafanikio yapo kwa yeyote yule anayehitaji, huwezi kufanikiwa kama huhitaji kufanikiwa ila wale watu wote wenye nia ya kufanikiwa mara zote hufanikiwa.. na wewe kuwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa, jiwekee njia za kufanikiwa na Tembelea ndoto zako Utafanikiwa tu..

Nakutakia mafanikio mema, Na endelea kutembelea shafiinad.com kwa kupata maarifa na makala ambazo zinatusaidia kwa kuweza kufanikiwa katika maisha yetu..

share ili wote tuwe ni watu wa kuwapa wenzetu motisha wa kufanikiwa...

share link kwa njia hizi hapa chini.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here