SHABAHA YAKO NI NINI? - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 28 May 2017

SHABAHA YAKO NI NINI?


Moja kati ya michezo yetu utotoni, tulikuwa tukichukua karatasi pamoja na kioo (aghalabu chenye lenzi), kisha tunakaa sehemu yenye jua kali. Basi, kile kioo ukikiweka kwa umakini, juu usawa wa karatasi huku mkono ukiwa umeutuliza kwa muda mrefu bila kuuhamishahamisha, ile karatasi huwaka moto. Sasa hiyo, ndiyo huitwa nguvu ya umakinifu. Halikadhalika katika maisha, mafanikio hufikiwa kwa shabaha makini kuelekea malengo husika (kama mtoto awekavyo umakini kwenye karatasi na kioo), kisha unapaswa kuvuta subira bila kukata tamaa wala kuhamisha malengo (kama mtoto atulizavyo mkono ulioshika kioo juu ya karatasi kwa muda mrefu bila kuuhamisha), mpaka mafanikio yatakapofikiwa (kama karatasi ilivyoungua).

Mafanikio bila shabaha makini ni sawa na kisa kifuatacho;
Yuko bwana mmoja aliyesafiri umbali mrefu hadi akafika kwenye njiapanda moja ndipo akasimama. Kisha akamuuliza mzee mmoja mpitanjia: "Kumradhi mzee, barabara hii inakwenda mpaka wapi?"

Yule mzee kwa busara na utii akajibu kwa kuuliza, "Kwani we unakwenda wapi?"

Msafiri akajibu: "Hata sijui, mi najiendea tu."

"Basi fuata barabara yoyote, utafika huko. Hapana tofauti yoyote alimradi uendapo ni popote!"


Ni kweli: Kama hujui uendako, barabara yoyote itakufikisha huko. Bimaana, kama huna shabaha maalumu katika kufikia malengo ya uwekezaji unaoufanya, bila shaka utaridhishwa na matokeo yoyote uyapatayo hata kama yatakuwa kiduchu kulinganisha na uwekezaji.

Hiyo ni sawa na kusema: Una timu kamili ya mpira wa miguu yenye wachezaji mahiri, wenye kiu na ari ya kushinda  dhidi ya timu yoyote. Lakini, mkiwa tayari uwanjani, mara unamwona refa anang'oa magoli ya pande zote mbili, kisha anaamuru mpira uanze. Kipi utafanya? Utakubali mpira uchezwe bila magoli? Na ukikubali, vipi utajua umepata goli (ushindi) ilhali shabaha haipo? Kimsingi; kiu na ari ya kufanikisha jambo fulani, kama haitokuwa na mwelekeo (shabaha) maalumu, ni sawa na kutaka makaa ya mgomba kwani hutopata kitu zaidi ya jivu tupu.

Kutoka fanani na hadhira page.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here