MUDA MWINGINE INAKUBIDI KUTAFUTA NJIA YAKO MWENYEWE. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 7 May 2017

MUDA MWINGINE INAKUBIDI KUTAFUTA NJIA YAKO MWENYEWE.Kila mtu anatamani kufanikiwa kwenye kile kitu anachofanya sasa kama ni biashara, kushawishi watu katika kununua bidhaa au huduma, kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa kwenye eneo lako la kazi, kufanikiwa kimasomo, kutumia kipaji chako, au kuwa mwandishi bora wa vitabu. Ni wazi kwa namna yoyote ile unavyotaka ufanikiwe kulingana na eneo unalotaka, kuna kila njia na kanuni muhimu unazopaswa kuzifuata ili kuhakikisha unafanikiwa kwenye eneo lako kama unavyotarajia.

Lakini leo hapa napenda kuzungumzia kutafuta njia ya pekee ya mafanikio, Naamanisha si lazima wote tuuze maji au wote tuimbe ila kama una kipaji cha kuimba basi si lazima ufuate vile watu wanavyoimba, unatakiwa ubuni njia ya kipekee itakayokupelekea kupata mashabiki wengi zaidi na kuwa wa kipekee zaidi.

kama wewe ni mchezaji, basi lazima uwe mbunifu ubuni style ambayo unaamini itawasumbua wenzako mpaka wewe ukaonekana uko vizuri katika namba yako, na ndio maana kila karibia ligi zote huko ulaya wachezaji huja na style mpya mpya kila mara hii ni kuwafanya wawe watu wa kubadilika na kuweza kuwa na mafanikio zaidi ya mchezo wao na wao kuwa bora zaidi katika timu zao.

Vivyo hivyo kazini, unatakiwa uwe mbunifu na sio kila siku unatumia uzoefu katika kufanya kazi, wakati mwingine unatafuta njia yako ya kufanya kazi ambayo unaamini itakuongezea ufanisi na kutoharibu matakwa ya kazi yako vile vile.
kama hupati njia, tengeneza yako

Na hata katika biashara, Kutoka kimaisha si kila mtu atatoka kwa mtiririko wa kitu fulani bali mtu atatoka katika maisha kwa njia yake ya kipekee, shida ni je utawezaje ijua njia unayoamini itakutoa kimaisha...?
Hapo ndipo wengi tunajikuta tunashindwa maisha na tunabaki kuwa wa kawaida au tukiamini kuwa hakuna njia ya sisi kufanikiwa zaidi ya kubakia kama tulivyo.
Ila mimi naamini kama wewe ni mfanya biashara ya magari usilazimishe njia za mijini maana wako wengi wewe peleka gari yako porini uwe una waleta watu mjini au laza gari huko inatoka asubuhi unakuja mjini hii itakufanya ujulikane na wanakijiji wa huko na taratibu utajitengenezea jina la mafanikio.
hivyo hivyo biashara zingine ni lazima ujue njia ya upataji kipato chako sasa na ujaribu kutengeneza njia mbadala ya hiyo ambayo unaamini itakuwa rahisi na ya kipekee katika kufikia malengo yako.

Amini ndugu yangu kila jambo linawezekana palipo na Mungu, hakuna jambo gumu zaidi kama utaweka juhudu yako kwanza.
Usipo amua kufanya leo, maendeleo yako pia yanasimama mpaka utakapoamua, hujachelewa ndugu yangu.
Amini Unaweza.

karibu shafiinad tukujuze zaidi.
kuwa karibu na facebook page yetu ya shafii blog.
na tembelea zaidi shafiinad.com upate kujua jalo vichache katika vile vya muhimu katika maisha ya leo na kesho.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here