JINSI YA KUJENGA MTANDAO WA BIASHARA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 28 May 2017

JINSI YA KUJENGA MTANDAO WA BIASHARA


Mtandao (network) ni muhimu sana katika kujenga biashara yako na katika kujijenga katika kazi/career yako. Mtandao unakusaidia kupata rasilimali, kupata taarifa za masoko, kupata taarifa mbalimbaili na kukamilisha mambo yako kwa urahisi. Ili kujenga Mtandao tunahitaji kufanya mambo yafuatayo:

1. Jenga mahusiano na watu ambao mnaweza kusaidiana kibiashara au kikazi. Mahusiano yanajengwa kwa kufahamiana na watu sahihi na kuwa na mawasialiano nao.

2. Shiriki katika matukio yatakayokukutanisha na watu-semina, mikutano, michezo, maonyesho, kusali, sherehe za muhimu, chakula cha jioni na vikundi vya msingi. Usijifungie sana.

3. Tengeneza utambulisho wako (business cards) na wa biashara yako (vipeperushi) na wapatie watu wanaoweza kuwa rasilimali kwako.

4. Tumia njia za kimtandao kuwasiliana na wateja wako, marafiki na jamii kwa ujumla (simu, email, instagram, blog, face book n.k). Uwe unajibu ujumbe na kufautilia mahusiano yako kwenye mtandao.

5. Tengeneza mtandao wa marefa wako (referees) ambao watakuwa mabalozi wako.Watu hawa wanatengenezwa kwa kujenga mahusiano ya karibu na hata kuwaomba wakutangazie biashara yako.

6. Uwe na takwimu/database za wateja wako na watu wa karibu. Kila kukiwa na matukio muhimu kama sikuu, kumbukumbu mbalimbali n.k wasalimu na kuwatakia kila la heri.

7. Toa huduma nzuri na jenga tabia ya kufuatilia jinsi huduma yako inapendwa sokoni. Kukiwa na bidhaa mpya au huduma yeyote mpya wajulishe wateja wako. Usikubali ukapita muda mrefu bila kuwa na kitu cha kukuweka karibu na wateja wako.

8. Kila unapopata fursa jitambulishe vizuri wewe pamoja na biashara yako. Kwa wanaotaka zaidi soma kitu kinaitwa “elevator speech” kwenye mtandao (http://www.businessballs.com/business-networking.htm ). Kwa kifupi kama uko sharp dakika 3 za kukutana na mtu kwenye lift zinatakiwa zitoshe kujitambulisha wewe na biashara yako na kupata mawasiliano ya mhusika.

9. Jenga tabia ya kusaidia watu wengine. Kabla ya kupokea jifunze kutoa, utapata mtandao mkubwa sana.

10. Timiza ahadi zako na uwe mwaminifu katika mahusiano yenu na kuhusu taarifa za wenzako.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here