JIFUNZE VITU VIPYA KILA SIKU. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 5 May 2017

JIFUNZE VITU VIPYA KILA SIKU.Katika maisha ya hapa Duniani, kila siku mambo yanabadilika kuanzia sekta ya afya, elimu na hata hali ya hewa duniani inabadilika..

vivyo hivyo hata katika maisha yetu binadamu kila siku kuna mambo mapya yanajitokeza ambayo yanatufanya kila siku tubadilike na tuwe na maendeleo ambayo tunaamini yanasababishwa na hali ya mabadiliko ya kidunia..

Leo hii kuna ugunduzi wa mambo mengi sana unafanywa na unaendelea kufanywa, ili tuweze rahisisha vitu na mambo ya maendeleo kwa ujumla. kwa mfano tumetoka kutumia watu kama nguvu kazi za kubeba vitu vigumu mpaka kutumia mitambo ya chuma kama winchi na hata robot kwa siku za hivi karibuni.

Kwa hiyo katika maisha ya mafanikio pia unatakiwa uwe mtu wa kujifunza kila siku.
unapojifunza mambo mengi unapata mwanga na wigo mpana wa mawazo na biashara ambapo utakuwa kila siku una buni na kupata faida kupitia wazo jipya ulilojifunza.

Wanasema "watu wenye mafanikio huwa wanajifunza jambo jipya kila siku, lakini watu ambao hawatafanikiwa wao huwa wanaona wanajua kila kitu."

Kwa hiyo unapoamua kuwa mtu wa kutafuta mafanikio katika maisha yako iwe mafanikio ya kiroho, kimwili, kibiashara na hata katika familia yako ni lazima uwe mtu wa kujifunza mambo mapya.
uendane na Wakati kwa kipindi ulichopo.
usipojitahidi katika kuhakikisha unafanikiwa utabakia kuteseka na kuamini umeumbiwa umasikini.

Unaweza soma mambo mapya kila mara kwa kupitia njia nyingi sana mfano sisi shafiinad.com tunatoa mafunzo ya kila aina bure tu kwa lengo la kukupa motisha au hamasa ili uweze kufikia maelngo yako, kuifanya ndoto yako iishi na iwe hai mpaka hapo utakapo ondoka katika sayari hii ya dunia.

Hakuna aliye anzia 100 kila mtu kaanzia moja japo tunatofautiana hiyo moja kuna wengine wao walianza fundishwa moja wakiwa wadogo na wengine tunajifunza moja tukiwa wakubwa na katika hali ngumu sana ya kujifunzia.

Ukisema Mo dewji amepewa mtaji unatakiwa ujue kakuta mtaji wa Tsh ngap na sasa ana Tsh ngapi hapo ndipo inapokuja point yangu ya kuwa kila mtu anaanza na moja yake tofauti ni mazingira ya uanzaji wa hiyo hatua ya kwanza.

Tembelea shafiinad.com kila siku ujifunze zaidi.

Amini Unaweza.
Kuthubutu ndio kuweza.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here