UNAPONUNUA KITU AMBACHO HAKIKUWEPI KATIKA MAHESABU, ITAKUBIDI UUZE KITU CHAKO CHA MUHIMU. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 22 May 2017

UNAPONUNUA KITU AMBACHO HAKIKUWEPI KATIKA MAHESABU, ITAKUBIDI UUZE KITU CHAKO CHA MUHIMU.

Maisha ya sasa yamekuwa magumu sana, hasa kwa sisi ambao tuna hali ya chini na tunatamani kujikwamua kwenda juu.
na kwa hali hii ya sasa iliyopo ni lazima tujitahidi kujilinda hasa katika matumizi ya kidogo tukipatacho ili tuweze kufika mbali, kwanini tuhangaike kutafuta alafu tuje kutumia kwa hovyo, bila malengo.?

Kwa hiyo leo hapa nataka kwa pamoja tuzungumze kuhusu matumizi yasiyo ya lazima katika vipato vyetu.

Kwanini ununue kitu ambacho hakikuwepo kwenye bajeti yako, huoni kama unajididimiza kimaisha.
mfano utakuta mtu ana 10000 ambayo hajaiwazia kununua kitu chochote ( iko nje ya bajeti ya matumizi ya nyumbani) lakini katika pita pita zake akakuta viatu vinauzwa, kwa vile ile pesa haikuwa na bajeti akaona bora anunue kile kiatu ingali viatu anavyo nyumbani ila kile kwa vile ile pesa haikuwa na kazi yake special akaamua kununua.

kumbe ile pesa angeweza kujiwekea katika bank yake ya kuhifadhia pesa, kama unawekaga 10000/= basi kwa siku hiyo ungekuwa umeweka 20000/=.

sasa kwa maisha ya kesho au ya baadae baada ya kununua hicho kiatu, inatokea una shida ya ghafla ambayo itahitaji hiyo pesa ili uweze kuitatua hiyo shida, kwa haraka haraka zaidi utajikuta unauza kitu cha ndani ili uweze kujisaidia kumaliza hilo tatizo.

hapa ndipo linapokuwa lengo langu kuwa kama usingalinunua kile kiatu maana yake ungalikuwa na pesa ya kumaliza hiyo shida.

kwa hiyo mimi nashauri kuwa usinunue kitu ambacho kipo nje ya bajeti au malengo yako katika pesa yako ili iweze kukusaidia kwa upande mwingine, Usiwe na tamaa ya kununua kila ukionacho mbele labda kiwe ni cha lazima..

Kwanini usiwe na malengo na matumizi yako ya pesa.?
Kwanini usiweze kufanikiwa kwa kujinyima vitu visivyo vya lazima.?
Kwanini ujikute unatoa kitu unachokipenda na cha lazima kwa ajili ya vitu ambavyo sio vya lazima.?


Tuamke wajasiriamali wenzangu,7 watafutaji wenzangu, ubahiri unafaa hasa katika sehemu hii ya matumizi ya pesa yasiyo ya lazima!!
Tujitahidi kutafuta pesa na tuwe watu wa kuogopa kutumia pesa.

Tuwekeze pesa zaidi katika kuzalisha na sio kuwekeza pesa katika kununua vitu ambavyo havina ulazima sana wa sisi kuwa navyo.

Kwa leo naishia hapa kwa vile sisi sote ni watu wa kuelewa na kufikiria hasa katika matumizi mabaya mazuri ya pesa.

Natumai u mzima wa afya, natumai na wewe ni miongoni mwa watu wanaopenda wenzao wafanikiwe, basi naomba share na wengine kwa njia hizi hapa chini au copy link na wape watu wengi wapate kujifunza kupitia shafiina.com.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here