UKIAMINI KUWA UPO SAHIHI, BASI ENDELEA KWA MAANA NI WEWE TU HAKUNA MWINGINE. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 22 May 2017

UKIAMINI KUWA UPO SAHIHI, BASI ENDELEA KWA MAANA NI WEWE TU HAKUNA MWINGINE.



Habari za uzima ndugu msomaji, Mjasiriamali mwenzangu, leo hii tunakutana tena hapa kwenye huu uwanja ni jambo jema la kumshukuru Mungu.

Leo nataka tupeane moyo, motisha juu ya uamuzi sahihi wa maisha yako na yangu.

Nataka nikuaminishe kama una imani na jambo lako basi huna haja ya kuogopa sababu tu kuwa watu wengi wanalikataa au wanakukatisha tamaa...
#KeepWalking  Imani yako ina ndoto kubwa sana ndani yake. Ina malengo makubwa sana,
ndoto yako Ina mpangilio wa kufikia malengo yako,
Lifanyie kazi hilo wazo au Imani yako, Kamwe usikatishwe moyo na watu wa pembeni yako.
Fanya kazi kwa nguvu, Ifanyie kwa ufasaha ndoto yako, Weka Imani yako juu( Endelea kuamini kile unachoamini).
Wanasema ndoto siku zote huja kwa yule anaye amini.
kwa hiyo basi amini kila kesho itakuwa nzuri zaidi ya leo.
 Mafanikio siku zote huenda kwa wale wanaotendea kazi ndoto zao, kwa kufanikisha ndoto zao maishani.
Usiangalie kipi kimekuja mbele yako kama kikwazo ila wewe songa mbele,endelea kutembea na ndoto zako,
Haijalishi mara ngapi umedondoka , umeshindwa kutimiza, we endelea kupambana kwa maana wanasema ukikosea mara 1000 maana yake umepata njia 1000 za kuweza kufikia malengo yako. 

Mheshimiwa Naibu waziri kigwangwala aliwahi andika na shafiinad.com nakuwekea hapa.

Kwenye maisha haya tunayoishi ukiwa na ndoto yako, ifanyie kazi. Usikate tamaa. Komaa. Haijalishi umekumbwa na dhoruba gani, ukaanguka - muhimu ni kwamba, inuka, kung'uta vumbi, SongaMbele! Usisimame, usikae, usilale....piga mwendo! Tembea! Songambele! Mafanikio makubwa yamo humu duniani miongoni mwa watu wanaopambana bila kukata tamaa! Ndoto yako hata iwe kubwa namna gani, iwe inahusu kitu kigumu namna gani, isimamie, ipiganie! Usikate tamaa.

Jaribu tena na tena! Kila ukianguka, inuka, jiulize, jirekebishe, jifunze, jipange upya, nenda tena! Hakuna kitu kikubwa kwako wala kigumu kwako.
Ni wewe na kichwa chako, na kemikali zako mwilini. Endelea kupiga mwendo! Usikate tamaa! Keep walking! Keep moving! Keep on believing!

Nami nasema amini ndoto yako.
Ifanye ndoto yako iishi.

Na pia wanasema Jambo baya ni baya tu hata kama linafanywa na watu wote, lakini jambo zuri ni zuri tu hata kama watu wote hawalifanyi.

kwa hiyo na wewe usiangalie watu wanasema nini juu ya ndoto yako.

we pambana kama unaamini na utashinda tu..

Hakuna linaloshindikana Kutoka kwa Mungu.


Tembelea shafiinad.com kwa makala nyingi zaidi ya hizi na pia utajifunza mambo mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here