WAZO LA BIASHARA YA MAZAO AU NAFAKA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 13 April 2017

WAZO LA BIASHARA YA MAZAO AU NAFAKA


Mazao hasa ya chakula ndio biashara kubwa sana na ya uhakika sana kwa maana kila mtu duniani lazima ale vyakula na ili aishi ni lazima apate vyakula vya kutosha. sasa katika nyanja za biashara kuna aina nyingi sana za biashara, kwa leo tu nataka kuelezea kwa ujumla biashara ya mazao ya kilimo na siku nyingine nitakua nachambua zao moja baada ya jingine katika kupata faida na gharama yake pia...

Leo hii tutaongelea sehemu kuu mbili, ya kwanza kwa wale wanaoanza mradi (Biashara) na wale wenye mtaji mkubwa wanaoweza nunua mzigo wa kutosha.

1. Kwa mtaji mdogo wa biashara. 

Tuongelee mahindi kama mfano mkubwa na mrahisi kuelezea katika jamii...
Mahindi wakati wa mavuno kwa mikoa kama ya Morogoro,Singida,Dodoma na mikoa ya jirani kama moshi huwa mahindi yanauzwa bei ndogo ambapo debe moja la mahindi (ujazo wa ndoo ya lita 20) huuzwa kwa Tsh 5000/= mpaka 7000/=. kwa maana hiyo kwa gunia la debe sita huuzwa 30,000/= mpaka 42,000/= na lile la debe saba huuzwa mpaka 49,000/=. kwa baadae baada ya muda wa mavuno, nafaka hiyo huanza kupanda bei na inategemea na mwaka ulivyo.
sasa kwa mtu mwenye mtaji mdogo kama mimi nilikoanzia nilinunua gunia 10 ambapo ilinighatimu karibu laki nne, (hii pamoja na upigaji wa dawa ya kuzuia wadudu). baada ya miezi mitano yaani kutokea mwezi wa saba mpaka wa 12 kila gunia nililonunua 30,000/= nililiuzwa kwa Tsh 60,000/= kwa maana nilipata laki sita (600,000/=) kwa maana hiyo nilipata faida ya laki mbili na kidogo. Je ni vip kama ukilima kidogo na ukanunua kidogo ukafikisha japo gunia 30 utakuwa umepata faida ya kiasi gani...?

Tujiwekezee kidogo kidogo tutaweza.
mi kwa sasa sipo katika ngazi hii nimepanda tena nimeanza biashara hii mwaka 2013 kwa mtaji huo.

2. Kwa wenye mtaji wa wastani na ule mtaji mkubwa.

Sasa katika mtililiko ule ule wa hapo juu, tuongelee kwa watu wenye mitaji ya kuanzia milioni tatu (3,000,000/=) na kuendelea. ambapo kwa kupata milioni tatu utakuwa na uwezo wa kununua gunia 100 za mahindi. kama mtu wa laki tatu aliweza pata laki sita kwa gunia 10 maana yake wa gunia 100 atakuwa anapata milioni sita (6,000,000/=) na hapo awali gunia kumi faida ilikuwa laki mbili hapa sasa faida ni zaidi ya milioni mbili.
je itakuaje kwa mtu mwenye mtaji wa milioni thelathini?
vip kwa mwenye kuwa na milioni zaidi ya mia moja...?

Maana yake the more mtaji mkubwa ndivyo hivyo hivyo faida nayo inakuwa kubwa. swala la kujua hapa ni kuwa unatakiwa upige gharama za dawa maana mazao kama mahindi yanahitaji upigaji wa dawa za kuua wadudu maaana huwa kuna wadudu wanakuja kuyaathiri mahindi. na pia gharama za upakiaji na ushushaji wakati wa kusafirisha.
Lakini amini usimamini kama una nia ya dhati unaweza anza kama mimi nilivyoanza na ukafikia malengo yako kama mimi kwa sasa nilipofikia...
Biashara ya mazao inahitaji mahali (location) kwa kukusanyia mzigo, kuhifadhia na pia sehemu ya kuuzia (soko).
Jitolee kwanza maana ukiwa mtu wa kutumia sana pesa huwezi fikia malengo yako. Unaweza fanya biashara ya kuzungusha mradi, mfano, unanunua mahindi morogoro unapeleka dar.
lakini kwa mtu mwenye mtaji wa laki tatu hii biashara huiwezi, kwa hiyo huna budi kuanza taratibu mpaka kufikia mzigo wa gunia japo mia moja ndipo unaweza fanya hii biashara ya kuzungusha bila kukaa na mzigo muda mrefu. shafiinad.com tunashauri uangalie wewe uwezo wako kwanza.

Faida ya kuzungusha ni kuwa utakuwa unapata faida kidogo kidogo kila siku na madhara yake ni kuwa unaweza uza mzigo elfu 60 ukarudi kununia ukakuta umepanda ni elfu 70.
hapo idadi ya mzigo wako utapungua tu.
Kwa hiyo kwa haya machache yangu, unaweza pata mwanga kidogo juu ya nini utakifanya. na usisite kuuliza jambo lolote hapa mimi nitakujibu bila wasiwasi.shafiinad.com tupo kwa ajili ya hilo.

wasambazie link hii wale unaohisi wanapenda kuona fursa.

Karibu shafiinad.com.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here