ONDOA HOFU YA WATU WA PEMBENI, JIANGALIE WEWE MWENYEWE NA ISHI NDOTO YAKO - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 17 April 2017

ONDOA HOFU YA WATU WA PEMBENI, JIANGALIE WEWE MWENYEWE NA ISHI NDOTO YAKO

Katika kanuni iliyowahi kutengenezwa na Dr. Daniel Gregory Amen kutoka jimbo la California nchini Marekani maarufu zaidi kama kanuni ya 18/40/60. Dr. Daniel anaelezea kanuni hii kuwa mtu anapokuwa na umri wa miaka 18 huwa kila wakati anawaza watu wanafikiri nini juu yake, hivyo kwa kila anachofanya akili na mawazo yake huwa yanajiuliza “watu wanatanionaje au watu watasema nini kwenye kile ninachotaka kufanya?.”

Lakini mtu huyo huyo akitimiza miaka 40 huwa hatilii maanani tena kuwa watu watasema nini juu yake na hapo anaamua kufanya kile alichokuwa anawaza kufanya bila kuwa na hofu ya watu. Mtu huyu pale anapofikisha miaka 60 anakuja kugundua kuwa hakuna mtu aliyekuwa akifikiri kwa lolote juu yake kwani kila mtu alikuwa anaangaika na maisha yake na kufikiri zaidi kujihusu yeye binafsi.

 Mara nyingi jambo hili linaweza kutokea kwa mtu yoyote yule mwenye kutaka kutimiza ndoto zake alizonazo. Watu wengi sana wametaliwa na hofu ya kutimiza mawazo mazuri waliyonayo ndani yao kwa muda mrefu hii ni kwa sababu ya kuwaza na kufikiri watu fulani watasema nini juu yao. Ukifatilia kwa umakini mkubwa utagundua mara nyingi hakuna mtu anayeweza kutoa muda wake mwingi kuwaza kwa ajili ya maisha ya mtu mwingine, kwani ukichunguza sana utaona kuwa kila mtu anafikiri juu ya maisha yake mwenyewe.

 Kufikiri watu wengine wanawaza nini juu yako ni kupoteza muda na fursa nyingi unazozipata katika maisha yako. Wakati mwingine tunapata mawazo mazuri ya kutukomboa kimaisha, mipango tunayojiwekea, tunatamani kuwa na vitu fulani na kufanikisha malengo tuliyonayo lakini tumewekewa kizuizi na mawazo mabaya yanayotudanganya akilini mwetu kwamba kuna watu wanatufatilia. Nataka nikuambie wazi kuwa hakuna mtu anayeweza kupoteza muda wake miwngi kwa ajili ya kufatilia wakati wote kile unachotaka kufanya.

You have to believe in yourself when no one else does. That’s what makes you a winner. -Venus Williams

 Ili ufanikiwe unahitaji kujiamini na kuiamini ndoto yako kwa kiwango cha juu usiku na mchana kuliko mtu mwingine wa pembeni yako. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwa kubaki akihofia watu wengine watamwonaje kwenye kile kitu anachotaka kufanya, ni lazima uelewe kuwa kila mtu ameumbwa kwa makusudi maalum na kupewa nfasi ya kuishi kwa ajili ya kutekeleza kusudi hilo hapa duniani.

Kama unataka kuwa mshindi kwenye ndoto yako ni lazima uamini uwezo ulionao kabla ya watu wengine kukuamini zaidi. Usipoteze muda mwingi ukijiona hauwezi katika kutekeleza jambo fulani unalotaka kulifanya. Wakati mwingine ni kawaida kabisa unapotaka kutimiza malengo yako watajitokeza watu fulani kwa ajili ya kutaka kukatisha tamaa, lakini unachopaswa ni kuiangalia ndoto yako na unapotaka kuelekea zaidi kuliko kutazama watu wengine wanasema nini.

Usikubali kukata tamaa kwa sababu upo kwenye mazingira ya watu wanaokukatisha tamaa, amua kusonga mbele na kuishi ndoto yako hata kama bado hauoni uwazi wa ushindi wako kwa sasa. Ni lazima kama unataka mafanikio juu ya ndoto yako uwe wa kwanza kujitoa kuiamini ndoto yako. Kumbuka hakuna umri maalum wa kuishi ndoto yako au kuanza kuamini unachokitaka. Wapo wanaosema nikifisha umri fulani nitaanza kufanya hiki au kile, lakini ukweli ni kuwa wanapoteza muda wao mwingi kwani muda wa kutimiza ndoto iliyo ndani yako ni sasa.

Usisubiri kila kitu kikae sawa kwako (perfectionism time) wala usisubiri watu wanaokusema wanyamaze na kukaa kimya bali unahitaji kuwaonyesha ujasiri wako kwa kuifata na kutimiza ndoto yako uliyonayo. Leo amua kusimama kwa ujasiri kwa kuifaata na kuishi ndoto yako pasipo kufikiri wengine watasema nini juu ya maisha yako.

Believe It’s Possible!

 Tembelea tovuti yangu kila siku upate mambo mapya

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here