NJIA UNAZO WEZA ONDOA VIRUS KWENYE SIMU YAKO - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 9 April 2017

NJIA UNAZO WEZA ONDOA VIRUS KWENYE SIMU YAKO
Kama unahisi simu yako ya android kuwa haifanyi kazi kawaida au inavirus, basi hizi hapa ni njia zitakazokusaidia kuondoa hao virus,


1, Ondoa app usiyo ielewa.

Kuipata na kuondoa app usiyoielewa nenda Settings then Apps au Application Manager. Angalia katika listi na angalia app ipi huijui na hukumbuki kudownload. Halafu gusa hiyo application ambayo unataka kudili nayo na itafungua “App Info screen”. Kwanza kabisa ondoa data cache za hiyo application kwa kubofya  "Clear Cache." Halafu delete data za application hiyo kwa kubofya  neno  "Clear Data." Baada ya kumaliza hili zoezi bonyeza "Uninstall" button na uiondoe app hiyo.

Baadhi ya application za virus zinaweza kuwa na administrator access na hapa itahitajika trick zaidi kuziondoa app za namna hii.

Kwanza ingia kwenye “safe mode” ya simu yako. Kwa kawaida sana kwenye simu za android, huhitaji kubofya kwa jumla kitufe cha kuzimia simu yako yaani "Power Off" au "Power Option" then menu zitatokea kama hivi. Kwa urahisi sasa ili tupate Safe Mode shikilia kwa jumla hiyo menyu mpaka neon “reboot in Safe Mode” litokee then bofya OK.

Mara baada ya simu yako kuwa katika Safe Mode, rudi sasa kwenye Apps au Application Manager na uninstall app yoyote iliyokuwa inakusumbua. Baadhi ya app za virus zina uwezo wa kuji install zenyewe kwa kutumia administrator status kwa hiyo utahitajika kuondoa hii ruhusa katika kifaa chako.

Nenda Settings > Security > Device administrators halafu tafuta app ambayo huwezi kuiondoa kwa kawaida, angalia kibox then chagua "Deactivate" katika screen >> select OK then rudi katika Apps au Application Manager kwa ajili ya ku uninstall.

Baada ya ku uninstalling app yako usiyoitambua au yenye virus, restart Android phone yako.

JILINDE MWENYEWE KUTOKUPATA VIRUS KWENYE SIMU YAKO.

Kama dalili za simu yako kuwa na virus zinavyosema, ili kulinda simu yako hakikisha una download na kuinstall app kutokea google play au katika source ambayo inaaminika hii itakusaidia kukulindia simu yako.

Pili, kuwa makini na websites na blogs unazotembelea, kudowload hovyo hovyo vitu kutoka sites zisizo aminika pia zinachangia sana kuweka virus kwenye simu yako. Shafiinda tuna kuhakikishia tupo salama tumejiunga na mtambo wa kusafisha kila kitu tunachokiweka hapa.

Na mwisho kila siku kuwa muagalifu sana maana virus huwezi muona akiwa anaingia u huwezi jua kama ndio unamchukua.

Unaweza share na wengine wapate kujua zaidi na unaweza share kwa kucopy link hii au kwa kubofya moja ya batani za social media zilizopo hapa chini.

Karibu shafiinad.com like fb page yetu kwa habari za maisha kwa haraka na urahisi.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here