NAMNA YA KUWALISHA KUKU KWA NJIA RAHISI. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 9 April 2017

NAMNA YA KUWALISHA KUKU KWA NJIA RAHISI.


Kuku ni biashara nzuri sana ambapo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikionekana ndio njia moja wapo ya kijasiriamali inayoweza kutuingizia kipato sana wa Tanzania na wa Africa kwa ujumla..

leo hii nataka niwaelezee ni namna gani mimi niliweza fuga kuku kwa urahisi hasa katika upande wa malisho.
mimi nitaongelea kwa singida nilivyokuwa nafanya na wewe utaweza tumia njia hii kukusaidia na utaweza fuga hata kuku elfu moja bila shida...

Wakati nafuga kuku wa kienyeji singida niliamua kuwafungia katika wavu kwa kuwagawa ili wasitoke toke nje na wasipigane wakati wa kula.
na ili kuweza kuwalisha vizuri bila shida niliamua kutumia njia hizi...

1. Kulima mahindi na alizeti pamoja na maboga.
Njia hii ilinisaidia sana maana katika mavuni niliyoyapata, mahindi nilichukua gunia na kujiuzia bei niliyoiona kuwa itanilipa kama kilimo as wengine wanavouza mahindi yao.
kuna wakati nilikuwa najiuzia hadi laki moja gunia na pesa hii nilikuwa naiandika katika daftari la kuku ili mwisho wa siku nije nione kwenye kuku nimepata faida gani.
lile gunia naenda kulikoboa napata pumba na mahindi hiki tayar ni chakula tena nimepata vyakula vya aina mbili.
nimepata pumba na mahindi ambavyo vyote kuku wanakula.
pia alizeti najiuzia kama mahindi then naenda kukamua mafuta then mafuta natumia na mashudu nawapa kuku wangu kama chakula..

hii ilinirahisishia sana kwenye kulisha kuku wangu maana nilijikuta napata fauda mara mbili ya kuku na kilimo (ndege wawili kwa jiwe moja). kwa hiyo njia hii ni nzuri sana.

2. Lakini pia unaweza ukawa unanunua mahitaji ya vyakula kwa jumla na ukaja tengeneza mwenyewe chakula chako mfano.
gunia la dagaa na sio vumbi la dagaa mwanza ni 70-85 elfu na mpaka kufikisha nyumban lets ashume laki moja, hapo ukapata gunia la mahindi, ukapata mashudu then ukawa unaandaa mwenyewe chakula chako utakuta bei ni chini sana kwa mtu mwenye kuku wengi hawezi ona hasara hata siku moja au kazi ngumu katika kuhudumia kuku wale.
kikubwa ni kuwa na mzigo wa kutosha ambapo utakaa muda mrefu na wewe kujikuta ukipata faida sana kw amuda ambao mzigo upo haujaisha...

na katika ufugaji wa kuku ni lazima uwe na uwezo wa kufikiria sana njia sahihi ya kuweza kuwalisha mfano.Kuhakikisha majani yanapatikana muda mwingi, chanjo na kinga na vitu vingine ambavyo kuku wanakula kama maboga. hii itakusaidia kuwa na upana wa chakula na kupelekea wewe kurahisisha kulisha chakula kuku wako cha aina moja kila siku.

ukibadilisha vyakula utawafanya wawe wazito na wawe na afya njema na kuuzika na kuzaliana kwa kasi sana...

leo naishia hapa.
kama hukusoma makala zangu za ufugaji wa kuku bofya hapa.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here