MATATIZO YA KIZAZI KWA MWANAUME NA TIBA YAKE. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 17 April 2017

MATATIZO YA KIZAZI KWA MWANAUME NA TIBA YAKE.
Kuna matatizo ya walio ndani ya ndoa ya kutopata mtoto na pia katika haya matatizo moja ya tatu ya watu wote wenye matatizo haya ni wanaume, na moja ya tatu tena ni wanawake na nyingine ni matatizo ya ki factor na sababu zisizo elezeka au kujulikana.

kama ulikuwa unajiiana bila kinga kwa muda wa mwaka sasa na hujapata mimba na una umri zaidi ya 30 ni vyema ukamuone Daktari, asilimia 65% ya wanandoa wanapata matibabu ya kizazi na wanafanikiwa kupata mimba, utafiti huu ni kutoka kwenye makala ya national infertility association.

Wataallamu wa maswala ya uzazi watawapima wote na leo tunaongelea mwanaume ambapo utaenda maabara upewa maelezo ya kuleta sample ambayo ni manii (shahawa) ili zije kupimwa.
kama utakuwa na tatizo litaonekana.
katika kipimo kuna vitu vingi utapimwa kuhakikisha majibu yanatoka ya kueleweka.
wanapima kuanzia uvutiko wa manii, uwingi wa mbegu, uhai wa mbegu, utembeaji wa mbegu, wanapima umbo la mbegu na n.k kwa hiyo katika hizo zote hapo ukikutwa na tatizo Daktari atakupa ushauri wa nini cha kufanya.
mara nyingine kuna sababu zinazofanya mwanaume ashindwe kumpa ujauzito mwanamke wake.

Sababu hizo kwa uchache ni.

LIFESTYLES FACTORS NA HISTORIA YA AFYA YAKO.

Kama unatumia style fulani ya maisha inaweza kukuletea shida katika kutungisha mimba.
mfano uvutaji wa sigara au bangi, unywaji wa pombe mara mbili au tatu kwa siku( wa kupitiliza) matatizo kama ya kuondolewa korodani, au dawa za kutibu arthritis, presha, cancer, au maambukizi katika korodani, uzito ulioptiliza, au magonjwa ambukizi ya ngono kama chlamydia au gonorrhea.

kama una moja ya haya mambo mwambie daktari wako ili aweze kukusaidia kuonheza chance ya kuweza tungisha mimba.

VARICOCELES.
 
Varicoceles ni ugonjwa unasababisha vein kuvimba ya kwenye scrotum na hupelekea joto kupanda katika korodani na hili joto lina leta madhara katika uzalishaji wa manii.

Dalili zake mara nyingi hazionekani ila baadhi huenda wakawa na maumivu ya kwenye scrotum yanatofautina makali katika wakati wa kukaa na kusimama au wakati wa mazoezi. (Daktari wako ataangalia hili tatizo pia)

Njia ya kutatua hili tatizo.
Upasuaji ili ku repair vericocele, au utumie intrauterine insemination (IUI) Au in vitro fertilization (IVF) ikiwa sambamba au hata isipokuwa sambamba na intracytoplasmic sperm injection (ICSI).

TATIZO KATIKA UTOAJI WA MANII.

Ili mwanaume uweze kumpa mwanamke ujauzito ni lazima ufikie ujazo fulani ambapo kisayansi kuanzia Ujazo wa Mls 2 ingawa wengine wana suggest mls 2.5 kwenda juu ndio utaweza tungisha mimba.
sasa wanaume wachache wana matatizo ya kuziba kwa njia ya kupitisha mbegu zisifikie katika maji maji(semen) ili zitolewe nje.
pia wanaume wengine hupatwa na matatizo ya ku enjaculate (kutoa manii) lakini yasitoke nje kupitia njia ya kawaida bali hukwama kwa sababu manii yanaingia njia ya mkojo na kutotoka nje kwa sababu shingo ya mfuko wa mkojo haufanyi kazi vizuri.

Maambukizi, ajali, kisukari, matatizo ya nerves yanaweza keta shida katika enjaculation process.

Dalili zake mara nyingi hazionekani ila kama una tatizo la kupeleka manij yako kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoa nje utaona wakati wa kukojoa ambapo mkojo utakuwa mzito na pia utaona unamwaga kiwango kidogo sana wakati wa kujaamiina au usione kabisa kama umetoa manij nje.

Njia ya kutibu ni IUI au Upasuaji kwa ajili ya kurekebisha njia iliyopelekea manii kuhama njia yake.
Tatizo lingine ni.

IDADI YA MBEGU AU UTEMBEEAJI WA MBEGU.( sperm count or motility problem).

Kwa kawaida mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni lazima awe na uwezo wa kuzalisha mbegu zaidi ya milion 20 inagawa wengine wanasema zaidi ya milioni 40 ukiwa chini ya hapo uwezekano wa kutungisha mimba huwa ni mdogo sana.
kwa hiyo ili uweze kutungisha mimba kirahisi lazima mbegu zako ziwe nyingi zaidi.
lakini pia unaweza zalisha mbegu nyingi na zikawa zimekufa hili ni tatizo lingine tena ambalo hutokana na sababu nyingi kama upungufu wa protein au utumiaji wa chemical zinazoathiri mbegu.

lakini pia ukiachana na kufa mbegu zinaweza zisitembee kwa sababu ya kukosa mkia mbegu ili ziogelee lazima ziwe na mkia, kama mbegu itakosa mkia maana yake haitaweza ogelea mpaka kufika kwenye yai na kupelekea kutokutungisha mimba.
na hii ya kutokuwa na mkia husababishwa na utumiaji sana wa sigara na chemical zinazo athiri mbegu.

Dalili hakuna katika hili.
njia ya kutatua tatizo ni kutumia fertility drugs kwa ajili ya kuzalisha mbegu nyingi, IUI au IVF sambamba na ICSI.

ANTI-SPERM ANTIBODIES.

mwili wako unaweza tengeneza kinga ambayo itakuwa inapunguza uogeleaji wa mbegu au kuharibu kabisa mbegu zako, hii hutokea sana baada ya vasectomy, au kutwist kwa korodani ndani ya scrotum, maambukizi au uvimbe.

hakuna dalili yoyote hapa na njia ya kutatua tatizo ni IVF sambamba na ICSI na hii ndio tiba ya kwanza lakini pia unawezw tumia steroids kama prednisone kuondoa kinga ya manii yako lakini pia daktari wako atakuandikia dawa nyingine kutokana na madhara ya aina flani ya dawa katika mwili wako.
mfani wengine hawatumii dawa zenye sulphur na n.k.

TATIZO LISILOJULIKANA.

Kuna watu wengine matatizo hayaonekani wakati wa vipimo vya manii kujua kama mwanaume huyu anaweza tungisha mimba au lah..

kwa hiyo daktari wako atapima kutokana na historia yako utakayompatia.
anaweza waza kuwa huenda umekuwa exposed katika mazingira yanayoharibu mbegu, au uwezo wa kutungisha mimba, kutakuwa na tatizo la kuzalisha mbegu labda hazikomai vizuri na n.k.
katika hili daktari wako atafanya utafiti mwingi zaidi juu yako kutokana na melezo yako ambayo yatampelekea yeye kujua sababu huenda nini...

lakini kikubwa kwanza unatakiwa ujue mzunguko wa mwenzako ili kujua ni lini itakuwa siku nzuri ya kutunga mimba kwake kabla ya kukimbila kwenda hospital.

Ogopa magonjwa ya zinaa kama kaswende na gonorrhea yakikaa sana baada ya maambukizi huua kizazi chako.
 
kama una swali la kuuliza uliza na kama una cha nyingeza nimesahau unaweza uliza.
shafiinad.com tupo hapa kwa ajili hiyo.
na somo lingine ntaeleza jinsi ya kupima manii na hii itakuwa kuanzia kukusanya manii yako mpaka majibu.
pamoja na matatizo ya wanawake.

Tovuti: www.shafiinad.com
E-mail: info@shafiinad.net

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here