Mambo ambayo yanakupotezea muda wako na yasiyo na faida katika maisha yako. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 1 April 2017

Mambo ambayo yanakupotezea muda wako na yasiyo na faida katika maisha yako.


Kila Binadamu Duniani ana nafasi katika maisha yake ya kuamua jambo na kulitekeleza, ila ili uweze kulitekeleza jambo lako ni lazima uwe na muda... na kuna vitu ambavyo tunavifanya vinatufanya tusifikie malengo yetu tulio jiwekea na haya mambo mara nyingi tunayafanya either bila kupenda au kwa kupenda bila kujua kama yanatu didimiza.

 1. KUTOKUWA NA VIPAUMBELE.
Kama wewe kila siku unaamka asubuhi unapanga mambo ya kuyafanya leo siku nzima (ushukuru kwa akili hiyo kwanza) bila kuwekeza hili jambo ni la kwanza na hili la mwisho na bila kuweka hili la muhimu na hili si la muhimu basi kila siku utajikuta hutimizi malengo yako na hii itapelekea kukata tamaa kwa vile utajiona huwezi.

2. KUSUBIRI KUPEWA NGUVU YA KUFANYA KITU MUHIMU KWAKO MWENYEWE.
Tujuavyo wengi ni kuwa ili ufanikiwe unatakiwa uwe na mtu anayekusaidia lakini si msaada wa pesa kama wengi tunadhania. hapa tuna ongelea msaada wa mawazo,ushauri na hata kuongozwa katika kufanya jambo lakini kama utatumia kigezo cha kutokufanya jambo kwa sababu tu umekosa mtu wa kukusaidia kamwe hutofanikiwa.

3. KUHOFU KUSEMWA NA WATU PALE UKISHINDWA.
Kama utakuwa unafanya mambo bila kuwa na hofu ya watu wa pemben watakuonaje daima utafanikiwa kwa sababu utafanya kazi yako kwa umakini,taratibu na utatimiza. lakini kama utafanya kwa kuhofia msukumo wa watu baki basi ujue utashindwa fikia malengo yako.

4.UOGA.
Jambo jema siku zote lina changamoto zake ambazo zinaweza kukuumiza kwa namna nyingi sana lakini naamini kama hutoweka uoga mbele kuthubutu jambo daima utafanikiwa tu. shafiinad.com msemo wetu ni To dare is to do. kuthubutu ndio kufanya. huwezi fanya jambo bila kuthubutu.

5. ULALAMISHI.
Kama kijana wa leo unatakiwa kutumia changa moto zako za maisha kama njia moja wapo ya kufikia malengo kiurahisi sana lakini kama utatumia njia ya kulalamikia matatizo yako maana yake kamwe huji kuyatafutia suluhisho ambalo litakusaidia kuepukana nalo na kusonga mbele zaidi...
na mambo mengine ni kama haya si lazima niyaelezeee.

i. kung'ang'ania kufanya peke yako kila kitu.

 ii. kutokuishi maisha yako na badala yake kuishi maisha kama ya fulani hata kama hafai kuwa role model wako.

 iii. Kurukia jukumu jipya kabla hujamaliza la awali.

 iv. kutaka kuiridhisha dunia na majirani zako.

 v. Kujilinganisha na waliofanikiwa zaidi yako, sio kwa minajili ya kupata changamoto bali kujikatisha tamaa.

vi. kutokujifunza kutokana na makosa uliyo yafanya nyuma. n.k

Kwa hiyo kama kijana mwenzangu nakusihi sana tukae chini tufikirie ni wapi tuna chemka ni wapi panapo tukwamisha then tukae chini tuombe washauri watushauri juu ya nini tufanye ili tuweze kujikwamua kutoka kwenye shida hii...

Kuna rafiki yangu mu holand alikuja field Turiani Hospital na jana tar 31/3 ameondoka nchini na b4 hajaondoka aliandika post fb iliyo elezea kila kitu alichojifunza Tanzania. na moja ya jambo aliloandika ni kuwa

"Vijana wa kitanzania wanaamini sana serikali yao kuwa ndio inayotakiwa kuwawezesha kimaendeleo, ingawa serikali pia ina changia katika kudumaza maendeleo ya vijana wao lakini vijana wa Kitanzania wanapaswa kuchangamka kujiinua pale walipo na kujitahidi kuijenga kesho yao bila kutegemea serikali yao ije iwawezeshe na hii ndio njia sahihi ya wao kuweza kufanikiwa kimaisha na kuondokana na dimbwi kubwa la ufukara walilokuwa nalo kwa sasa".

 kwa mantiki hiyo mtu aliyekuja Tanzania kwa miezi mitatu tu ameweza kuona hili swala lakini viongozi wetu na wasomi wetu wameshindwa kututatulia na kutuelekeza juu ya jambo hili...

Vijana tuamkeni, Maisha yanaenda mbio sana na uzee ni mgumu kumeza. Maana Ukijua kilichomo ndani yako basi we ni tajiri.

 nakutakia mafanikio mema. Sambaza kwa wengine wapate kuona na kujisomea mawazo yangu ambayo yanaweza saidia wengi kama yalivyonisaidia mimi.

shafiiad.com

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here