KITABU KIZURI KINAWEZA BADILI MAISHA YAKO, A GOOD BOOK CAN CHANGE YOUR LIFE - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 7 April 2017

KITABU KIZURI KINAWEZA BADILI MAISHA YAKO, A GOOD BOOK CAN CHANGE YOUR LIFE

Habari za muda huu mpendwa msomaji wa makala zangu, natumai mzima wa afya, leo nipo hapa kukupa motisha ya jinsi gani kitabu au vitabu kwa wingi vinavyoweza kubadili maisha yako... na nitapenda kuzungumzia aina ya vitabu na sio kutaja kitabu lengo hasa ni la kukupa mwanga zaidi wa kutafuta aina za vitabu uvipendavyo.. ningependa tuelewe kuwa vitabu vingi vina maneno mengi mazuri na unachotakiwa wewe ni kuwa na uwezo wa kutafakari jambo ndipo utaona uzuri wa kitabu hicho. napenda nizungumzie aina ya vitabu ambavyo vitakutoa kwenye dimbwi la ufukara na ujinga na kukuleta katika kuona ndoto yako na kuitekeleza.
 Aina za vitabu ni.

 1. Vitabu vya mafunzo ya ujasiriamali.
Hivi ni vitabu vingi sana na vizuri vipo vingi vilivyoandikwa na wakongwe wa uandishi na matajiri duniani wengi wao wakielezea jinsi walivoanza mpaka kufanikiwa kuwa mabilionea...
vitabu hivi vina makala nyingi sana na hasa vinakupa motisha ya kujaribu na huwa wanaeleza ni biashara gani kwa mwaka wao ilikuwa marketable na nini wanafikiria mbeleni. wanakupa changamoto nyini sana za wewe kujitahidi kutoka hapo ulipo mpaka kufikia ndoto yako ambayo ndio unawaza... Mfano wa waandishi wa hivi vitabu ni Robert kiyosaki (Mwanzilishi wa kampuni ya RICH DAD POOR DAD) nitaweka kitabu chake hmu kupitia shafiinad.com na hii kampuni aliianzisha baada ya kuandika kitabu cha poor dad, rich dad na kikauza sana ndipo akaona kumbe ni fursa na madam jina limekuwa kubwa basi akalifanya kuwa ndio jina la kampuni. wengine ni Donald Trumph Rais wa marekani ambaye ana elezea sana mikakati yake ya biashara za real estate na jinsi alivyoweza fanikiwa. wapo wengi ila hao ni mfano wao.

2. Vitabu vya kukupa motisha.
Vitabu hivi ni tofauti na vitabu vya kuelezea ujasiriamali na ingawa waandishi ni wapo wanaojirudia wameandika ya ujasiriamali na wakaandika vya motisha na n.k. Sasa katika vitabu hivi vipo vilivyokuwa vinakupa motisha katika fani fulani na vipo vinavyokupa motisha uamini tu kuwa unaweza fanya jambo flani.
vitabu hivi ni vizuri sana ukivisoma kwa maana vinakupa hamu ya kujaribu kwa kile walichokieleza ndani. mimi wakati na soma kitabu cha believe u can, nilipata hamasa sana na nkajikuta naamini kweli ntaweza na sasa nataka mwenzangu na wewe usome vitabu hivyo uweze kupata mwangaza zaidi. najua watanzania au wa afrika tunasifika kwa kutopenda kusoma vitabu ila amini ndugu yangu vitabu vinabadili maisha yako.

 3. Vitabu vya Uongozi katika Maisha yako.
Simaanishi uongozi wa kiserikali, hapana naamaanisha uongozi wako wewe katika kufikia malengo yako, kuna kitabu kinaitwa How to archive your goals. hiki ni kitabu kinachokupa mwongozo wa namna gani unaweza fikia malengo yako na hasa katika time management na katika matumizi hasa ya pesa zako. vitabu vya namna hii vina base kukushauri na kukuelekeza namna gani wewe utaweza fanikiwa...
ni vitabu vingi sana ukitafuta utavipata ambavyo vina weza badili maisha yako na msimamo wako katika maisha. ntaviweka baadhi ya vitabu hapa mtavipakua bure.

 4. Vitabu vya imani na mafanikio.
Vitabu hivi vinajihusisha na imani za kumuamini Mungu ambapo mimi naamini huwezi fanikiwa kama hakuna Mungu katika maisha yako, kila kitu ni kwa ajili ya Mungu. Sasa basi vitabu hivi vinabase sana katika kukuelezea njia sahihi zaidi za kumtukuza Mungu na wewe kuweza kufanikiwa katika maisha yako.
viko vingi ila katika hivyo nilivyosoma nilpenda kitabu cha without God, No success kinaelezea vizuri sana.jaribu kutafuta utafurahi na mimi ntavipakia humu ninyi mtadownload free(Bure)..
Vipo vitabu vya aina nyingi sana kama vilivyo upande wa pesa tu na n.k lakini mimi napenda kwa leo niishie hapa na hakika utakuwa umepata mwanga kidogo wa kwanini watu tunashauriwa tusome vitabu vyenye mafanikio kwetu na sio hadithi za magazetini na mitandaoni ambayo hutupa akili ya kufikiria ujinga badala ya kuwaza ntatokaje katika dimbwi hili la shida. simaanishi usisome hadithi za vichekesho bali weka na muda wa kusoma sana vitabu vyenye dira za maisha.
 Shafiinad.com tuko hapa kuhakikisha unapata mwangaza wa maisha katika kile tunaamini kinaweza kukusaidia kufanikiwa.
 Amini unaweza.
kuthubutu ndio kuweza.

Tovuti: shafiinad.com
E-mail: info@shafiinad.net/com

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here