Jinsi ya kujua simu yako kama imeingiliwa na virusi. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 9 April 2017

Jinsi ya kujua simu yako kama imeingiliwa na virusi.

shafiinad.com

Mara nyingi tumezoea kuona computer zetu zikiwa zimevamiwa na virus, lakini ukweli ni kuwa hadi simu zinavamiwa na virus na tena ni rahisi sana kwa sababu wengi hatujui dalili zake na hii hupelekea kukaa kwenye simu kwa muda mrefu na kutuharibia mafaili yetu...

leo nawapa dalili za kuwa simu yako imevamiwa na virus na hizi ni dalili za kawaida sana kutokea katika simu zetu.

1. Data zinatumika sana.
Alama ya kwanza hapa ni hii ya kuona matumizi ya kifurushi chako cha MB kinaisha haraka sana bila kutegemea hii ni kwa sababu virus wanajaribu kuna run kazi kwa ndani na kuunganisha na internet, kama huna unlimited data plan hii itakukost na kula hadi pesa zako shafiinad.com tutakufundisha namna ya kudhibiti Mb zako...

2. App ku crash mara kwa mara.
Hii ni alama ya pili ya kujua kuwa simu yako imevamiwa na virus, ambapo kila wakati simu yako itakuwa ina cresha app fulani ulizofungua na ku stuck kwa muda mwingi hii inasababishwa na virus katika simu yako.

kwa hiyo ukiona hii dalili jua tayari wameingia hawa jamaa na wanaharibu system yako.

3. Pop-ups zisizoeleweka.

Ingawa kuna website ambazo zinakuja na pop up au kwa njia nyingine naweza sema maandishi hutokea kwa juu baada ya kifungua website fulani,(shafiinad.com hatuna ukiziona si zetu hizo zikatae) basi na virus wana pop-up ambapo wanaweza kuja kwako kwa kupitia baadhi ya links.
mfano ukiona links inasema simu yako ina virusi usipende ku click hiyo link mara nyingi ndio virus wenyewe hao..

4. App ambazo hukuzihifadhi na zipo.
Kuna baadhi ya virus wanaingia kupitia app za watu na hii inasababisha wao kufanya kile wanachojisikia..
mfano kama huu hujawahi install app yoyote kuhusu kitu fulani lakini ukaikuta. jua ndio ishara ya kuwa virus wamevamia simu yako...

kikubwa ni kuwa makini na app unazo weka na vitu unavyo download ambavyo vinaweza kuwa na virus vitakusumbua baadae lakin shafiinad app iko salama kabisa...


5. Kuisha kwa better haraka.
Tunajua kuwa smart phone zetu zinakula chaji pale tunapozitumia au kuweka data hewani mara nyingi chaji huisha hasa pale ambapo tumelazimisha 3G na huwa kawaida ukizima data chaji huchukua muda mrefu.
lakini kwa hawa jamaa wakishaingia kwenye kifaa chako(simu) kwa hiyo ukiona betri yako haikai na chaji hata kama umezima data jua tu tayari kuna virus na wakati mwingine hata kama umewasha data kuna kiwango cha kuliwa betri kikizidi ujue wapo hawa jamaa....

Nitakuja elezea njia za kuwaondoa virus katika simu yako na kaa karibu na shafiinad.com tukupe makala za maisha, Biashara na teknolojia kama hizi...

wasambazie link na wengine wapate kujua na kukwepa virus katika simu zao.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here