Amini unaweza kufanya, Believe u can do. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 6 April 2017

Amini unaweza kufanya, Believe u can do.Katika maisha ya Hapa Duniani, kila mtu huwa na uwezo wake wa kufikiri na kuamua jambo litakalompa mafanikio na hii hutokana na asili ya nguvu alizopewa na muumba wake...
Sasa tunapofika katika mambo ya kuamua kufanikiwa hapa wengi huwa tunatamani sana kufanikiwa lakini hujikita tukiishia kujenga nyumba angani bila hata ya gharama...

kuna mambo mengi sana yanayopelekea iweze kutokea hivo na mambo haya yanawezekana kukwepeka kama tu utatilia mkazo mambo yako ya msingi na ukaacha ambayo sio ya msingi...

mfano wewe unataka kufanikiwa katika kilimo, wengi wetu tusiosoma tunaamini kilimo ndio kitatutoa na ndio hali halisi kuwa kilimo ndicho uti wa mgongo wetu.
sasa basi ili uweze kufanikiwa katika kilimo fulani lazima uchukue muda wa kujifunza na kukielewa vizuri kabla hujaanza kulima,
hapa wengi wetu tunajikuta tunavamia kilimo bila hata ya kujifunza zaidi.
mfano watu wanalima zao la vitunguu kipindi cha masika, wewe bila kujua ukaingia kulima amini una asilimia chache sana za kuvuna kwa sababu hutajua ni lini muda wa dawa na zipi dalili zinazohitaji dawa...

hivyo hivyo kwenye maisha ya kawaida.
usipende vamia kitu kisa tu umepewa hadithi ya mafanikio ya mtu fulani kupitia hicho...

hapa nashauri kuwa ili uweze kuwa mtu wa kutimiza ndoto zako lazima upende kujifunza na ujifunze kiundani zaidi ili ukitoka na wewe uwe mwalimu na si mwanafunzi wa hilo jambo tena...

fuata hizi njia utafanikiwa hapa nakupa njia tatu tu ambazo ni strong kwa ajili ya kufanikiwa kwako...


1. Kuwa mbunifu.
Kuna kipindi watu wanajikuta wanaona mwenzake kafanikiwa ye hafanikiwi katika biashara moja na eneo moja, mwisho wa siku unajikuta unashindwa ndoto zako..

kama wewe unataka kuanzisha duka na jirani yako ana duka we kuwa specific kuwa utakuwa unauza nini hasa kitakachowafanya waje.
jirani anauza maharage,sukari,mchele,mafuta n.k kama tujuavyo basi we ili uweze kushindana nae kibiashara we kuwa specific uza mchele tu tena hakikisha ni wa ubora wa juu.
hapa mwisho wa siku yeye mwenyewe atakuja nunua kwako.
au mwenzako kila anapata faida ya 200/= we punguza 150/= hapa utapata watu wengi zaidi na faida itakuwa haraka kuliko yule wa 200/=.

2. Acha kulalamika.
Watu wengi sana tumekuwa na tabia za kulalama sana hasa pale unapojikuta umeshindwa jambo fulani.
mi kwa upeo wangu naona umefika muda sasa wa kuacha kulalama na kuchukulia kukosea kwetu ndio njia sahihi ya mafanikio.
bila kukosea huwezi tengeneza kitu bora zaidi na ili uwe mtu mkubwa katika jambo lako lazima ukosee mara nyingi nyingi ndipo utatoa product bora zaidi.
kwanini ulalamike wakati uwezo unao.?

3. Amini katika Mungu. Believe in God.
Baadhi yetu watanzania tuna imani mbaya sana ambazo zinatufanya tushindwe kuendelea.
mfano watu wawili wakifanya biashara moja then mmoja akatapa wateja wengi sana kuliko mwingine watu huanza kusema yule anayepata wateja wengi ana dawa ya kuvutia wateja.
swali kwanini na wewe usiende tafuta yako.
hapa ninachojifunza ni ufinyu wa akili katika jambo ulilolianza.

biashara inahitaji ubunifu na sio uchawi, ukiona mwenzako anamafanikio katika biashara zake we huna budi kujifunza toka kwake. angalia ni wapi amekuzidi mpaka wateja waende kwake, then jirekebishe halafu boresha zaidi ya yeye.
mfano anauza kilo Tsh 500/= kwa faida ya tsh 100/= we shusha kidogo kwa faida hata ya hamsini, kama yeye ana lugha nzuri ya kuvutia wateja na wewe jifunze customer care zaidi.
Believe me, uchawi wa kwenye biashara ni ubunifu wako tu.

Hutoendelea kama wewe ni mtu wa kulia lia na imani potofu.

Nikutakie siku njema na mafanikio mema huko uliko.
Lakini kumbuka kila jambo lina mkono wa Mungu, Amini leo na jifunze jambo baadae ukithubutu kulifanya utaamini ya kuwa hakuna uchawi ila kunahitaji akili ulopewa na Mungu uitumie ipasavyo.
shafiinad.com

like page yangu ya facebook kwa kubofya hapa.
Pakua app yetu kwa kubofya hapa.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here