AMINI SIRI HIZI ZINAWEZA KUKUSAIDIA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 9 April 2017

AMINI SIRI HIZI ZINAWEZA KUKUSAIDIA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO.


Katika maisha yetu kila mmoja huwa anatamani sana kufanya jambo fulani na kufikia malengo yake, na ndoto hizi watu wengi sana tunazo lakini huwa tunajikuta tunashindwa kwa sababu nyingi tu.
hapa mimi nataka kukupa baadhi ambapo naamini wengi zinatufelisha ambazo zina uhusiano na jamii yako inayokuzunguka...

Siri zenyewe au sababu za wewe kushindwa kufanikiwa ni hizi hapa katika jamii yako kama ukitaka kuwa kiongozi au kufanya biashara.

1. Kuwa rafiki wa watu.
Usipende kukosoa na kulaumu watu walio karibu yako hii itakusaidia wao kukuona unawajali na kuwaheshimu.
kuwa mpole,wakubali wanachofanya na waambie kistarabu kama kuna jambo wanakosea.
kuwa msikilizaji mzuri wa mawazo yao, penda kuongelea jambo ambalo wanalipenda na wafanye wajisikie wao wana umuhimu sana kwako.

2. Washinde watu katika njia yako ya kufikiria.

njia sahihi ya kukwepa kugombana na watu ni kuogopa ugomvi, pia penda sana kuheshimu jambo alilofanya mtu wako wa karibu, usiseme kuwa amekosea au hauko sahihi direct ila tumia njia nyingine ya kumuelekeza jambo hilo, pia wacha wenzako  wajione wazo lile ni lao au lake yule anayeongea na sio kumuambia kuwa hilo wazo lilikuwa la fulani, kubali mawazo yao ya biashara, unganisha mawazo yako na tambua challenge zako ili iwe rahisi kufikia malengo.

3. Kuwa kiongozi wa mawazo na busara.
katika jamii ili uweze kuiteka jamii yako na wakupende ili wewe ufanikiwe lazima uwe mtu wa kuwakubali, kuwaeleza makosa yao indirect, ongelea kwanza makosa yako au mapungufu yako kabla hujayasema ya wenzako, wahifadhie mabaya yao na uyaseme yale yao mazuri na wafanye wenzako wawe na furaha katika maamuzi yao.
hii itakufanya kukubalika sana na kukurahisishia kufikia malengo yako.

4. Jifunze kupambana na uoga.
Mara nyingine kuna uoga wa aina nyingi sana unatuvamia wakati wa kutafuta mafanikio ili uwe na maisha mazuri na yenye kujiweza kipesa lakini tunakuwa na uoga.
na moja ya uoga katika jamii zetu ni kuogopa kuchekwa pale utakaposhindwa na hii hutokana na wewe kujigamba katika jamii yako kwa kile ulichokuwa unakifanya na kuwadharau wengine.

4. Njia sahihi ya kuondoa uoga wa kuthubutu ni kusali.
Katika makala zangu siku zote nawaambia watu kuwa bila Mungu hakuna kitu kitakachotupeleka mbali.
ili uondokane na uoga wa kuanza ni kumtanguliza mungu tu hakuna namna nyingine...

Mwisho naomba niseme kuwa kama unataka kufanikiwa katika jambo lako ni lazima ujifunze zaidi kuhusu hilo jambo na kuanza pale unapojiona upo tayari kulianza...

ogopa kufanya jambo kwa kuiga...

Tovuti: shafiinad.com
E-mail: info@shafiinad.net

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here