UREMBO VS MALEZI YA FAMILIA NA WATOTO - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 27 March 2017

UREMBO VS MALEZI YA FAMILIA NA WATOTO

Asilimia kubwa ya wanawake wanashindana mavazi na mambo yote yanayohusu urembo, mfano mavazi,vipodozi na mambo mengine mengi sana ambayo yapo katika kuwapendezesha wawe na muonekano tofauti na wengine au tofauti na asili yake. ,kama wanawake wangekuwa na mashindano ya malezi bora na mashindano ya ndoa bora na tamu basi Dunia ingekuwa sehemu nzuri sana kuishi.maana nguvu wanazotumia kuhakikisha wanapendeza ni nyingi kuliko nguvu wanazotumia katika malezi ya watoto wao na malezi ya ndoa zao pia...


utakuta mwanamke yupo busy kuvaa akitaka kushindana na jirani yake ambaye mwenzie ana hangaika kuelimisha watoto wake na kuhakikisha ndoa yake iko imara haiteteleki. huyu ndiye mwenye akili za maisha na hasa za kujenga nyumba yake..

 simaanishi wanawake wasijipodoe wapendeze hapana mi nnachotaka ni wanawake waweke nguvu pia katika kujenga familia zao na kuwajenga watoto wao katika maadili mema

 Hakuna mashindano ya wanawake yanayohusu malezi bora ya watoto ,na mashindano ya malezi bora yangekuwepo basi tungekuwa na kizazi cha dhahabu kwa tabia bora za watoto na utamaduni mzuri wa Mtanzania na mila na desturi. Mapenzi ya dhati na ndoa zenye furaha ni chache sana siku hizi ila tiba ni kumpenda na kumuheshimu mkeo/mumeo.
 Ni kuongeza nguvu katika kumpenda mumeo/Mkeo na kuhakikisha kuwa mnakuwa na furaha ndani ya ndoa na hii si kwa kupendeza tu ni kazi ya ziada inayohitaji umakini na ustaarabu ili uweze kutekeleza majukumu yako yatakayopelekea ndoa yako iwe nzuri na imara.

.Je, una watoto? Basi, wafunze nidhamu.Wafundishe utii tangu utoto wao.

je, una watoto wa kike? Wafunze usafi wa mwili,lakini usiwabembeleze mno.

Enjoy life with your wife
 #Nakupenda mke wangu

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here