URAFIKI NA MARAFIKI WENYE FAIDA KATIKA MAISHA YAKO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 25 March 2017

URAFIKI NA MARAFIKI WENYE FAIDA KATIKA MAISHA YAKO.Binadamu karibu wote duniani tuna marafiki na hawa marafiki wameletwa na urafiki wetu. Sasa kuna aina nyingi sana za marafiki tulionao ambao wanatuzunguka sisi kwa ujumla. wapo ambao wana faida na sisi na wapo ambao hawana faida na sisi katika maisha yetu ya Duniani na pia juu kwa muumba wa vyote (kwa wenye kuamini). Kwa hiyo leo hapa nataka niwape kidogo mdokezo wa marafiki na urafiki ambapo mada hii niliikuta mahali mtu ameandika anaitwa fanani japo aliandika kwa ufupi lakin ni vyema sana tukashirikishana wote tukafaidika na maada hii. Ni bora kuwa na marafiki wa aina tatu katika maisha yako yote ili kuwa mtu mwenye mafanikio ya kiroho,kimwili na kiakili katika ustawi wa maisha bora kabla uzee haujapiga hodi.Tafuta marafiki wafuatao......

1.Rafiki aliyekuzidi umri na mwenye nguvu ya kiroho ili akusaidie kukujenga kiroho na kukufunza kutizama mambo kwa jicho la tatu.

2.Rafiki aliyekuzidi utashi ,maarifa na elimu ili akufunze kutanua misuli ya ubongo kwa kukufunza namna ya kufikili na kutunza kinywa kwa kuzungumza mambo ya msingi na kuwa na bidhaa adimu adabu, na hekima na busara.

3.Rafiki mwenye mafanikio ambaye atakuwa chachu yako ya kuwa na njaa ya mafanikio na darasa la kujifunza kuwa na malengo thabiti na yenye tija katika maendeleo yako na kutimiza malengo yako. tembelea zaidi blog hii utajua mengi zaidi na mazuri kwa ajili ya maisha yako ya sasa na huko mbelen uendako. shafiinad.com tunakupa kila kitu kizuri ambacho tunaamini utakiweza kukifata nankukufanya ufanikiwe zaidi.

Acha kutumia muda mwingi kujadili watu na kulalamika sababu uzee usio na maandalizi mema ni mgumu kuliko ujana wenye starehe.Good friends care for each other. Close friends understand each other, But true friends stay forever..beyond words, beyond distance, beyond time…! Kwa hiyo acha kujaza marafiki fb acha kujaza ma group whatsapp yasiyokijenga kwa chochote. iwe kimwili au ki roho ili uweze kuwa na mwisho mzuri... Ahsante na karibu tena katika blog yangu ya shafiinad.com

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here