Njia 6 Rahisi za kuondoa manyama tumboni, Kulingana na Sayansi - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 15 March 2017

Njia 6 Rahisi za kuondoa manyama tumboni, Kulingana na SayansiMwanamke kuwa na manyama ya ziada tumboni sio ndio kuwa hana afya.
Ni ukweli kuwa kuna watu wengi ni wanene na wana afya nzuri tu.  
Kinyume chake, wengi ambao si wanene ni wana uzito wa kawaida lakini ndio wanamatatizo ya metabolic.
Hiyo ni kwa sababu mafuta chini ya ngozi ni kweli si kwamba yanaleta matatizo makubwa.
Ni mafuta katika nafasi ya tumbo ambayo husababisha masuala makubwa.
Kama una mafuta mengi ya ziada kuzunguka kiuno chako, hata kama wewe si mzito sana, basi unapaswa kuchukua baadhi ya hatua ya kujikwamua na hiyo shida.
MFANO WA MANYAMA UZEMBE TUMBONI

Mafuta ya Tumbo kwa kawaida hupimwa kwa kuzungusha kipimio katika kiuno chako.

Hii inaweza kufanyika kwa urahisi nyumbani na kipimo cha tape kile cha mafundi cherehani.
na majibu yako yakiwa juu ya inchi 40 (102 cm) kwa wanaume na inchi 35 (88 cm) kwa wanawake, basi hapo kitaalamu tunaanza kuita abdominal obesity (uzito wa tumbo uliopitiliza).
Ni kweli kuna mikakati michache yakuthibitika ya kuhakikisha watu wanapunguza manyama uzembe katika tumbo zaidi kuliko sehemu nyingine za mwili.
Hizi hapa ni njia 6 za kuhakikisha unapoteza hayo mafuta yalozidi katika tumbo lako.

1.Usile sukari na epuka vinywaji vyenye sukari sukari.

Kuzidisha sukari ni hatari kwa afya yako.Tafiti nyingi sana zinaonesha madhara makubwa sana katika metabolic health, Sukari ina Glucose, fructose, na fructose pekee inaweza kumeng’enywa na ini katika kiwango kinachohitajika. Pale unapokula kiwango kingi cha sukari, ini linapata mzigo mkubwa sana wa fructose na inalazimika sasa ini kupeleka fructose kwenda kwenye fat.
Tafiti nyingi sana zinaonyesha kuwa kula kiwango kingi cha sukari mwilini kunapelekea kuwepo na kiwango kikubwa cha fructose ndani yake na hii fructose inazalisha mafuta ambayo kwa kiwango kikubwa huenda kukaa kwenye nyama za pembeni za tumbo.
Sukari inayopatikana katika kimiminika kama juisi ni mbaya sana kwa sababau sukari hiyo haitambuliki mara nyingi na ubongo sawa na calories ambazo si za kimiminika, kwa hiyo wakati unakunywa kinywaji ambacho ni kitamu, maana yake mwisho wa siku umekunywa calores nyingi pia ndani ya mwili wako

Kumbuka kwamba kuna matunda ambayo ni matamu na yana sukari ambayo ipo kwa kiwango kidogo na ambacho kitatumika katika mwili na pia kuna baadhi ya matunda ambayo yana fibers ndani yake ambayo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula mfano ndizi.

Kama unataka kupunguza ulaji wa sukari, basi lazima kwanza usome maandishi ya hicho chakula au kinywaji chako. Hata vyakula ambavyo huuzwa kama vyakula vya afya vinaweza kuwa na sukari ya kiwango kikubwa.

2. Kula zaidi protini kwa muda mrefu ili kupunguza mafuta ya tumbo.
BAADHI YA VYAKULA VYA PROTEIN
Protini ni moja ya aina ya vyakula muhimu zaidi linapokuja suala la kupoteza uzito na manyama uzembe ya tumboni.
Imekuwa ikionesha uwezo wa kupunguza kwa 60%, kuongeza umeng’enywaji wa kalori 80-100 kwa siku.
Kama Umekuwa na lengo la kuondoa uzito na manyama uzembe ya tumboni basi moja ya njia nzuri na sahihi ni kula vyakula vyenye wingi wa protein kama ndio mlo wako. Hii itakusaidia sana kupoteza uzito na manyama uzembe pia.

Si tu ni kukusaidia kupunguza manyama, bali pia inaweza kukusaidia kuepuka na kujirudia rudia kwa uzito na manyama pia kama wewe utaamua kula vyakula hivyo milelel.
Pia kuna baadhi ya Tafiti wana hakikisha kuwa protein ndio inayopigana zaidi na mafuta katika mwili.

Hivyo fanya jitihada za kuongeza ulaji wako wa vyakula vyenye high-protini kama vile mayai, samaki, dagaa, kunde, karanga, nyama, maziwa na baadhi nafaka ambazo ni za protein. Hivi ni vyanzo bora vya protini katika mlo.

3. Punguza kiwango cha kabohydrate Katika mlo wako, ni njia nzuri sana ya kupunguza mafuta.
 
Hii inakubaliwa na tafiti mbalimbali. Wakati watu wakipunguza kula carbohydrate na mafuta yaao hushuka na kuweza kupoteza hadi kilo.
Zaidi ya majaribio 20 yamedhibitisha sasa kwamba mtu akila kiwango cha chini cha wanga  hupungua uzito mara 2-3 zaidi kuliko mtu anayechukua mlo wenye kiwango cha chini cha mafuta.
Hii ni kweli hata wakati wa utafiti kuna makundi yaliyopewa nafasi ya kula kiwango cha chini cha wanga na kuna makundi yaliyo takiwa yasile vyakula vyenye mafuta na wakae njaa. Na ilionekana wale wanaokula wanga kidogo waliweza kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kuliko wale walio kaa na njaa. Hapa tunajifunza njia si kukaa na njaa njia sahihi ni kupunguza kiwango cha kula wanga katika miili yetu.
Epuka wanga uliyosafishwa (mikate, pasta, nk) Itakuwa vyema sana kama utaweka protein iwe juu zaidi ya wanga.
Hata hivyo, kama unahitaji kupoteza uzito haraka, anza kufikiria kuacha wanga au punguza chini ya gramu 50 kwa siku. Hii itauweka mwili wako katika hali ya ketosis, na kufanya mwili wako kuanza kuchoma mafuta yaliyopo mwilini mwako kuzalisha nguvu.
Pia kupunguza wanga mwilini si tu unapunguza unene, na pia utakuwa umejikomboa kutoka katika madhara ya kupatwa na mashambulizi ya ugonjwa wa kisukari. 

4. Kula vyakula tajiri katika nyuzi (fibers), mfano ndizi. 

BAADHI YA VYAKULA VYENYE FIBERS

fiber ni kichocheo zaidi cha mmeng’enyo wa chakula katika mwili wa binadamu.
Ni muhimu sana kula fibers lakin cha kujua ni kuwa sio fabers zote zimetengenezwa sawa.
Fibers hizi zina bind na maji na kutengeneza thick gel ambayo itaenda kukaa kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (gut).
Na hii gel inapunguza movement ya chakula katika tumbo lako na kupunguza mmeng’enyo wa chakula na ufyonzwaji wa nutrients. Matokeo yake utakuwa unahisi kushiba kwa muda mrefu na kupunguza hamu yakula.
Moja ya tafiti zinaonyesha kuwa watu wanaotumia gram 14 kwa siku za fibers wana punguza kiwango cha calories katika mwili kwa asilimia 10% na kupunguza uzito wa hadi kilo 2kg((4.5 lbs) ) kwa muda wa miezi mine (4).
njia bora ya kupata nyuzi zaidi ni kula vyakula kama mboga na matunda. Mikunde pia ni chanzo kizuri, kama vile baadhi ya nafaka kama shayiri.

5. Mazoezi ni madhubuti sana katika kupunguza mafuta ya tumbo.

BAADHI YA MAZOEZI

 Mazoezi ni muhimu kwa sababu mbalimbali. Ni miongoni mwa mambo bora unaweza kufanya kama unataka kuishi kwa muda mrefu, na kuwa na maisha ya afya na kuepuka magonjwa pia. Hata hivyo, kukumbuka kwamba mimi si zungumzii mazoezi ya tumbo hapa. yaani kupunguza (mafuta katika tumbo tu) hilo swala haiwezekani, ila naaminisha kuwa ukifanya mazoezi hata mafuta ya tumboni yanaweza kupungua.
Katika utafiti mmoja, Ulionesha kuwa mazoezi hayapunguzi kwa kiasi kikubwa sana kiwango cha mafuta mwilini lakini inaaminika kuwa mazoezi nayo yanapunguza kwa kiasi chake kama utafata na aina ya vyakula pia.
Mazoezi yanapunguza uvimbe, kiwango cha sukari mwilini (umeshasoma hapo juu madhara ya sukari mwilini) na hata katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ambao unahusiana na mfumo central obesity.


6. Kufuatilia vyakula yako na kufikiri hasa unakula nini na katika kiwango gani cha vyakula.

Hapo juu nimeelezea ki vipi manyama uzembe au kitambi hutokea katika tumbo na nimetoa hadi na njia bora za kula na kuishi ili uondokane na kitambi.
Sasa basi ni kazi yako sasa kuwa makini na vyakula vyako, wakati ukinunua kitu au kula kitu hakikisha unaweza kujua ni kiwango gani mfano cha sugar katika hicho chakula, kiwango cha protein,wanga na n.k
Lengo hapa ni usipitilize kile kiwango sahihi ambacho unatakiwa kula kwa siku, na ili ujue viwango vya nutrient kila bidhaa huandikwa katika package yake na katika vitu kama matunda mara nyingi matunda huwa yana kiwango cha wastani cha nutrient ambazo haziwezi muathiri mtu.
Kwa hiyo Kaa fikiria, amua sasa kuanza,ondoa manyama uzembe tumboni.
Elimu hii inatolewa bure kabisa na wala sifundishi njia ambazo haziwezekani na huhitaji kununua kitu kwangu.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here