MAONO NA THAMANI YA MAONO KATIKA MAISHA YAKO - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 29 March 2017

MAONO NA THAMANI YA MAONO KATIKA MAISHA YAKO

Nimevutiwa sana na hii makala nimeona na mimi niwashirikishe ninyi ili kwa pamoja tuweze kujua maana ya maono na uwezo wa kutambua ono lako... THAMANI ya kitu ipo ndani ya kitu chenyewe, yaani kwa mfanoTHAMANI ya fedha ipo KATIKA fedha yenyewe.SASA basi, unapoyaendea maono yako ni wazi umeona THAMANI iliyondani ya maono hayo japo inawezekana wengine hawawezi kujua. Kumbuka maono yanakuwa ndani yako kwa hiyo usimshangae anayekupinga au anaona unapoteza muda.
1. Hajui asili ya maono yako kabisa.
2. THAMANI ya maono uliyo nayo si rahisi kila mtu kuyajua.
3. Mwanzo na mwisho Wa maono mwingine haujui kabisa hivyo kupingwa ni jambo la kawaida kwa mtu aliyebeba maono.
MUHIMU: Hapa ninaongea na kila mmoja wetu kwa maana ninajua mtu humu ana maono ambayo ndio kusudi lake kuwepo hapa duniani.Sasa kwa kuwa watu hawajui asili ya maono yako ujue ni wazi utapata CHANGAMOTO kubwa sana. Siku moja shafiinad.com nikiwa mtoto niliwahi hisi katika gari wenye raha ni abiria tu na si Dereva.
Mbona Dereva anahangaika hangaika tu wala hapumziki anabadilisha badilisha tu gia kila wakati, kwa kweli niliona hana raha kabisa.Nilikuwa ninaona kila hatua anayoiendea anabadili gia tena akifika katika miinuko miinuko ndio anabadili mara kwa mara.  Nilipokua mkubwa nikagundua yafuatayo. Safari ya Dereva inaendana na maono.
Sisi kama abiria tunaweza kulala kwa kuwa tuko na mbeba maono, lakini Dereva kwa kuwa ndiye mbeba maono hawezi kulala hata kidogo na ukiona ameanza kusinzia sinzia ujue ajali inakaribia.Sasa tega sikio kama mbeba maono kwa kuwa umekwisha kuona mwisho wa maono yako unaanza kukutana na upinzani.Kuna upinzani wa nje na upinzani wa ndani.
1.   Upinzani wa ndani ni ile hali ya NAFSI yako mwenyewe hasa kwa kuona ni kama unataka kushindwa au kukata tamaa vile.
2.   Upinzani wa nje huambatana na mazingira na watu wanaokuzunguka wewe.

Wengine wanaweza kuwa na mtazamo hasi na unachokifanya Lakini kwa kuwa unaasili ya maono ndani yako kuna NGUVU akupazo MUNGU aliyeweka maono ndani yako kiasi cha kutoka kwenye hali ya raha na kuanza kukabili CHANGAMOTO, na wakati mwingine utaona hata watu wa karibu wanakushambulia. Pia unashindwa kuelewa kabisa. Msukumo wa ndani ya nafsi yako unaweza ukawa pengine chini na watu wa nje wakiongeza unaweza ukaona kama hutofika katika maono yako. Lakini kwa kuwa unaasili ya maono ndani yako kuna NGUVU akupazo MUNGU aliyeweka maono ndani yako kiasi cha kutoka kwenye hali ya raha na kuanza kukabili CHANGAMOTO, na wakati mwingine utaona hata watu Wa karibu wanakushambulia pia na hata unashindwa kuelewa kabisa. Kwa kuwa wewe tu ndio unayajua adui wa aina yoyote ile, ataanza na wewe kwanza na si mwingine, lakini ile hamu ya kuyatimiza na kufika mwisho itakupa nguvu za ajabu kuelekea ushindi mkubwa wa maono yako. Maeneo matatu unayopatia NGUVU  Ni MUNGU mwenyewe kwa kuwa ameianzisha kazi na anataka uitimize katika mapenzi yake.Msukumo chanya uliopo ndani yako unaolenga wewe kufanikiwa juu ya maono hayo. Watu uliopewa kukusaidia katika maono yako watatumika kukuinua.KUMBUKA: SHUJAA BILA VITA SI SHUJAA Na unapopitia CHANGAMOTO ili kunolewa vizuri kuelekea mafanikio yaliyo mbele yako MUNGU atakupa tumaini na Amani mpaka ufike mwisho Wa maono yako. Kwa hypo hayo ni maeneo muhimu sana ambayo hukupa nguvu sana kuelekea maono yako.

1. Jenga uhusiano mzuri na MUNGU akupaye maono.
2. Uwe na Uwezo Wa kugeuza hasi kuwa chanya nyakati zote, haijalishi mazingira yakoje.
3. Tunza urafiki na watu wote na zaidi wale uliopewa mtimize maono pamoja. Kwa hiyo hayo ni maeneo muhimu sana ambayo hukupa NGUVU KUELEKEA maono yako.share na comment pia kama mada imekupendeza au kukufundisha jambo.


No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here