MAISHA NA MUZIKI, SOMA UGUTUKE. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 25 March 2017

MAISHA NA MUZIKI, SOMA UGUTUKE.

Ushabaki kitu cha ajabu sana; mtu analipa pesa yake ili akamsikiliza msanii akiimba, cha ajabu, kufika ukumbini sasa, msanii anaimba mstari mmoja halafu anawaelekezea mic mashabaiki na kuwataka waitikie. Mashabiki nao, kama majuha wanalipuka wakiuitikia wimbo huo kwa nguvu kuliko hata msanii mwenyewe, mpaka unashindwa kuelewa nani aliyelipwa kuimba. Ukute sasa na msanii mwenyewe anataka kuwapasua makoromeo; eti yeye ndiye ameshika mic, lakini anaimba kijimstari kidogo tu, mathalani, "Ameota mapembe, mwongezee mkia...!!..." Kisha anawasikilizia mashabiki. Salaale, waliolipa ili waimbiwe, wanalipuka utadhani wao ndo wamelipwa kuimba, "...NA UKINIBEEP TU NAKUPIGIA, AND LEMME KEEP ONE THING CLEAR, BLAH BLAH BLAH SITAKI KUSIKIA, S'O SIMBA S'O CHUI S'O CHUI S'O MAMBA...HAAAA, NGOZI YANGU INATOSHA KUJIGAMBA...HHHAAA!..."😂 Mpaka show ikaishe, msanii aliyelipwa kuimba anaondoka ukumbini hata jasho la pua halijamtoka, na sauti iko saaaafi utadhani amekunywa mayai mabichi. Kisanga kinabaki kwa mashabiki sasa, waliolipa pesa ili waambiwe, wanatoka ukumbini hoi bin taabani, sauti zinawakoroma kama vyura wa majurubani. Kama huo si ujahili, tuuiteje basi? Ujinga wa mashabiki ndiyo faraja ya msanii. Unakuta msanii ana msongo wa mawazo; pengine hana pesa, au ameachwa na mpenzi wake, sasa kwa hasira anaamua kusema hataki mpenzi, au hataki kuoa. Kama haitoshi, kwa hisia kali anaamua kuandika na kibao kabisa. Kama alivyofanya Juma Nature alivyoandika "SITAKI DEMU", au kama alivyofanya Diamond alipoandika " MAPENZI BASI" au MwanaFA alipoandika "BADO NIPONIPO". Ujinga wa shabiki sasa; unakuta mshabiki yeye hana msongo kama wa msanii wake; yeye ana pesa zake, hana maumivu ya kuachwa, umri umeshakwenda, walakini, ghafla tu ati naye hataki kuoa. Ukimuuliza kwanini? Atakwambia "Bado niponipo kwanza" au "sitaki demu". Kutahamaki, miaka saba imekatika; Diamond aliyeimba "Mapenzi basi" yungali mapenzini japo siyo na Wema tena, MwanaFA aliyeimba "Bado niponipo kwanza" naye tayari amekwishaoa, na Juma Nature aliyeimba "Sitaki demu" sasa ana demu japo siyo tena yule Sinta. Sasa mshabiki anaanza kuhatahata, kama aliyezinduka toka usingizini au aliyezikuliwa toka kaburi, ndiyo naye sasa anataka kuoa, lakini pesa zimemwishia na mchumba amemkimbia. Na kwakuwa hana tena pesa ya mahari wala ya kuhonga, sasa anabaki kujifariji kwa wimbo mpya wa mwanaFA "Dume Suruali" HujakomaTu? Acha kufuata mkumbo. *Wenzako wanapasua anga, we unakaza na kamba* 😂 #Kalagabhaho

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here