KISA CHA MUUZA SAMBUSA NA MSINGI WA MAFANIKIO YAKO. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 26 March 2017

KISA CHA MUUZA SAMBUSA NA MSINGI WA MAFANIKIO YAKO.

Katika maisha kila mtu huwa na mtazamo wake tofauti na hutegemea sana na aina ya mawazo yake ambayo pia huzalishwa na uwezo wake wa kufikiria na kuchambua mambo yaliyo ya msingi na ambayo si ya msingi katika maisha yake... leo napenda tuangalie kisa kimoja hivi ambacho shafiinad.com tunawaletea kutoka kwabmwandishi maundu mwingizi ambaye ameamua kutushirikisha hiki kisa kizuri na sisi tupate kupanuka kiakili na mawazo.... kuna utafiti umetolewa unaonesha mpaka kufikia mwaka 2030 asilimia kubwa ya ajira hasa kwa wanaume zitakuwanzimepungua sana kutokana na ukuaji wa sayansi ya maroboti n akupelekea kutumika sana kuliko binadamu... sasa basi soma kisa hiki then jiulize utapendelea kuwa upande upi ambao ni mzuri kwako..? Palikuwapo na muuza sambusa mashuhuri jijini Arusha. Mgahawa wake ulipakana na kampuni moja kubwa. Kutoka na ladha murua ya sambusa zake, wafanyakazi wengi, kama si wote katika kampuni anayopakana nayo, kila siku walifika mgahawani pake kununua sambusa. Siku moja, meneja wa kampuni naye alifika mgahawani kununua sambusa. Akiwa anaendelea kutafuna sambusa yake, alimuuliza muuza sambusa, ambaye ndiye mmiliki wa mgahawa, "Bwana Sajam, mbali ya kuonesha umahiri katika upishi, pia umeshihirisha uhodari wako katika utawala hata ukaweza kuukuza na kuuboresha mgahawa wako kiasi hiki. Hivi, hauoni kama unapoteza muda wako mwingi na kipaji chako kwenye kijibiashara kidogo cha kuuza sambusa? Hebu fikiri, kama ungekuwa umeajiriwa kwenye kampuni kubwa kama mimi, saa hizi ungekuwa meneja mwenye mafanikio makubwa mno." Muuza sambusa alitabasamu huku akiendelea kupanga sambusa zake, kisha akasema, "Mimi nafikiri biashara yangu ni bora kuliko kazi yako. Unajua kwanini? Miaka kumi iliyopita, nilianza biashara ya kuuza sambusa kwenye kikapu kidogo kwa kuwazungukia wateja. Kipindi hicho nawe ndiyo ulikuwa umeajiriwa rasmi. Wakati huo mimi nilikuwa nikijipatia shilingi elfu moja kwa mwezi mzima, na wewe ulikuwa ukilipwa shilingi elfu kumi kila mwisho wa mwezi. Ndani ya miaka hii kumi, sote tumepitia mabadiliko makubwa; mimi nimeondokea kuwa muuza sambusa mashuhuri ninayemiliki mgahawa wangu, ilhali wewe umepanda cheo na kuwa meneja. Kwa sasa, wewe unalipwa milioni moja kwa mwezi, nami pato langu kwa mwezi ni hiyohiyo milioni moja na wakati mwingine napata juu ya hapo." Meneja akiwa hajaiona tofauti ya kipato baina yao hata muuza sambusa yule akasema biashara yake ni bora zaidi, bwana Sajam aliendelea kufafanua: "Hebu itazame kesho ya wanangu halafu ulinganishe na ya wanao - nilianza maisha kwa adha ya mtaji mdogo wa biashara. Lakini, mwanangu hatokuja kupitia hayo tena. Ikifika wakati mwanangu akaja kuichukua na kuisimamia biashara hii, hatohitaji kuanza alifu kwa kijiti. Ataendeleza mgahawa na kuuboresha zaidi. Tofauti na wewe, ambapo mafanikio ya kampuni unayofanya kazi, yatakwenda kwa watoto wa bosi wako, na si kwa wanao. Na kamwe, hautoweza kumpa mwanao hicho cheo cha umeneja akiendeleze, kama atataka itambidi naye aanzie sifuri ili kuitafuta miamoja. Kama ambavyo wewe ulitaabika kwa miaka kumi kufikia cheo hicho, mwanao naye atahitaji kutaabika miaka mingi kutafuta nafasi kama hiyo. Sasa hebu tazama, wakati mwanangu anaanzia hapa nilipoifikisha biashara yangu, mwanao wewe atakuwa ndo kwanza anaanzia safari ya sifuri kuyatufa mafanikio. Na mpaka akafikie kuwa meneja, atamkuta mwanangu akiwa mbali mno. Haya, niambie nani anapoteza muda na kipaji chake baina yetu?" Meneja alilipia sambusa aliyokula, na kuondoka bila kuaga. ***Imeandikwa na Maundu Mwingizi (Mwanabalagha). Kama lipo ulilojifunza, unaweza kuLike, kuComment ka kuShare.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here