Kanuni 10 za kupunguza uzito kwa njia rahisi na salama. - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 15 March 2017

Kanuni 10 za kupunguza uzito kwa njia rahisi na salama.Uzito katika mwili wa binadamu ni hatari kama utazidi kiwango kinachokubalika kiafya, madhara ya kuwa na uzito uliopitiliza ni kama kuumwa miguu hasa magoti kwa kushindwa kubeba kiwili wili chako, hormone imbalance(kutokukaa vizuri kwa homoni), na magonjwa kama kisukari na presha pia hayatokuwa mbali na wewe.
 
kwa hiyo ni lazima wewe kama unajijali afya yako uweze kujidhibiti na uzito uliopitiliza ambao unaweza sababishwa na mafuta kuwepo mengi mwilini.
sasa hapa nimekupa dondoo kidogo tu za kuweza kuukimbia uzito ulio pitiliza.
 
1. Kula Vyakula vyenye wingi wa protein.

    Kifungua kinywa kinaonesha kina punguza hamu ya kula na kupunguza kiwango cha kula calories kwa siku.

2. Epuka vinywaji vya sukari na juice ya matunda iliyoongezewa sukari.

    Hivi ndio vitu vyenye mafuta zaidi unavyoweza kula kama utatumia hizi juisi, na kuepuka nazo kutakusaidia kupunguza mwili na uzito pia.

3. Kunywa maji nusu saa kabla ya kula.
    Kuna tafiti inayoonesha kunywa maji nusu saa kabla ya kula inaongeza uwezekano wa kupunguza uzito kwa asilimia 44% kwa muda wa miezi 3.

4. Chagua vyakula rafiki kwa kupunguza uzito.

    Baadhi ya vyakula ni muhimu sana kwa kupoteza au kupunguza kiwango cha mafuta mwilini,
Baadhi ni mayai, mboga za majani ya kijani,Samaki wanaotoa mafuta(salmon), nyama ya kuku,Viazi mbatata vilivyo chemshwa,maharage na kunde, supu, parachichi, apple,karanga mafuta ya nazi na hata maziwa mtindi.
 
5. Kula vyakula vyenye fiber (soluble fiber).
    Tafiti zinaonesha kuwa kula vyakula vya fibers vinapunguza mafuta, hasa mafuta ya kwenye tumbo. Supplements za fibers kama glucomannan zinasaidia pia.

6. Kunywa chai au kahawa.

    Kama wewe ni mnywaji mzuri wa kahawa au chai, basi kunywa zaidi ya uwezavyo maana ndani yake kuna caffein inayosaidia kuongeza ufanisi katika mmeng’enyo wa chakula.

7. Kula sana vyakula ambavyo havijapikwa.

    Pendelea aina ya vyakula ambavyo havijapikwa ama havijapikwa sana, vile ni vizuri kwa afya yako na pia havisababishi ulaji wa kupitiliza kwa maana hutavipenda saana na hii itapelekea ule kwa kiwango kidogo tu na kumbuka vyakula kama mboga za majani,karanga na hata parachichi ni vizuri kwa afya yako.
 

8. Kula chakula chako taratibu, ulaji wa chakula kwa haraka kuna ongeza uwezekano wa kupata uzito uliopitiliza.

Kula chakula kwa taratibu bila kuwa na haraka, inakufanya ushibe vizuri na ina boost hormone zinazohusika na upunguzaji wa uzito mwilini.

9. Tumia sahani ndogo wakati wa kula,

    Tafiti nyingi zinaonesha kuwa watu wengi wanaotumia sahani ndogo wakati wa kula huwa wanakula kiwango kidogo pia cha chakula. Inashangaza lakini ndio ukweli na hufanyika.

10. Pata usingizi mzuri wakati wa kulala usiku kila siku.

      Upungufu wa usingizi ni miongoni mwa factor hatari ambayo inapelekea kuongezeka kwa uzito ingawa watu huamini kujitesa kwa kutokulala ndio kupungua hii si kweli na haina ukweli wowote zaidi ya kuongezeka uzito, kwa hiyo kuwa na usingizi wa kutosha kutapelekea uwe na uzito wa kawaida.
Tembelea tovuti yangu mra kwa mara upate udate nyingi na nzuri kwa ajili ya makala za afya, ujasiriamali, teknolojia na hata mahusiano.
Tembelea na ulike page yangu ya Facebook kwa kubofya hapa.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here