NIDHAMU YA FEDHA. NA NDIO SABABU ZA WATU KUFANIKIWA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 3 January 2017

NIDHAMU YA FEDHA. NA NDIO SABABU ZA WATU KUFANIKIWA

Fedha,Pesa au hela ni neno zuri sana kila mtu anatakamani kulisikia na kuwa nalo lakini ni ngumu sana kuwa nalo kama hutokuwa na nidhamu nalo...
hivi ndivyo mimo ninavyoanza kuelezea nidhamu ya pesa katika jamii zetu...
Watu wengi waliofanikiwa wamefanikiwa kuwa sababu tu wana nidhamu ya pesa...KWANINI NIDHAMU YA PESA

Pesa ni kitu adimu sana na ukikipata kinahitajika kila mahari na ili uweze kuwa nazo lazima ujichunge katika maamuzi yako ya kuitumia hiyo pesa la sivyo utajikuta unaanguka mara kwa mara..

NIDHAMU YA PESA NI KAMA HIZI.

1/ TUMIA KWA VITU VYA LAZIMA.
Pesa wanasema ni mwana haramu kwa sababu ukiwa nayo tu unajikuta unajihisi mtu mwingine kabisa maana utajiona kama vile kila kitu unaweza kuwa nacho...
ni kweli lakini ukwel wake ni mbaya kwa baadae..
sasa lazima ujue kujichunga kitu kipi cha lazima na kipi si cha lazima ili uwekeze pesa kwingine na izalishe nyingine zaid lakin ukitumia tu zitaisha na hutaweza kuwekeza...

2/PENDA KUWEKEZA ZAID.
Kila unapopata pesa usikimbilie kutumia tu kwa maaana kutumia kunakufanya usizalishe nyingi zaid na hapi utajikuta unatumia pesa hiyo hiyo unayoingiza kuliko kuongeza chanzo na mwisho wa siku unajikuta huongezeki katika kile unachoingiza kila siku..
mfano mwajiriwa kila siku mshahara ule ule mpaka anastafu hana kitu lakin angewekeza maana yake angepokea mshahara na faida katika kuwekeza kwake angekuwa na kipato kikubwa zaid ya kile cha mshahara tu...

3/JIFUNZE UBAHIRI.
Ubahiri watu wanasema sio mzuri kwa vile hurudisha watu nyuma lakini mimi nasema ubahiri mbaya ni ule wa kuweka pess ndani na kuacha zisizaliane kwa kuwekeza na ubaya wa ubahiri ninaongelea hapa ni wa kutoa toa pesa kwa watu mfano unakuwa na mwanamke pembeni unamuhonga pesa ovyo ovyo huku ni kujifilisi...
shafiinad.com najua
umekuwa kwenye mkutano na watu kumetokea mchango unakimbilia kutoa ili watu wakuone huu ndio ujinga ambao unatakiwa uogope sana ili uweze kuwa na pesa...

4/ JIFUNZE KUWEKEZA AKIBA.
Katika mambo muhimu sana katika maisha ya uhuru wa pesa ni kujua na kudhubutu kuweka pesa kidogo kwa ajiri ya kazi isiyojulikana kwa baadae ambayo itakuja kunyanyua biashara na kukusaidia pale shida ya haraka inapotokea badala ya kwenda kuchukua kwenye chanzo chako cha pesa...
na umaweza ukaweka akiba kiasi hata vha asilimia 10 kile mwez au kutokana na kipato chako hii itasaidia sana na ndio nidhamu ya mtu anayetaka kuwa na pesa...

5/ MUINI MUNGU KATIKA KILA KITU CHAKO
M/Mungu ndio kila kitu katika hii dunia na ndio mpaji wa riziki zetu za kila siku, kw ahiyo ili uweze kufanikiwa unatakiwa utumie njia sahihi za utafutaji wa pesa sio kisa unataka pesa utumie mfano shafiinad.com nakupa hizi njia  uwizi,utapeli,unyang'anyi na hata ufisadi hapo utakuwa umechemka maaana hutakuwa huru na pesa zako..
kikubwa hapa ni kufanya njia sahihi ya kutafuta pesa ambazo zitampendeza M/Mungu na kutokuwa na shaka kwa wakazi wanaokuzunguka...

Kwa leo naishia hapa unaweza tafuta zaidi NIDHAMU YA PESA kila siku kwa kufikiria nankuchunguza kwa nini watu wanashindwa sana kial siku katika kufikia malengo yao ya kuwa huru na pesa...

Shafiinad.com
Karibu tujielimishe mambo mengi,Fursa,technologia,afya na mengineyo mengi tu...

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here