MATUMIZI MAZURI YA MUDA, NA NDIO CHANZO CHA MAFANIKO KATIKA MAISha yako - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 17 January 2017

MATUMIZI MAZURI YA MUDA, NA NDIO CHANZO CHA MAFANIKO KATIKA MAISha yako


Leo nataka tuzungumze  kidogo katika kipengele cha muda...
hasa katika matumizi mazuri yamuda ili kuweza kufikia malengo yako...
watu wengi sana wameshasema maneno mengi sana kuhusu muda wengine husema muda ni pesa na wengine husema mengi zaidi...
hapa leo nataka tuambiane katika matumizi ya muda ili uweze kuwa mtu wa kufanikiwa katika mambo yako..
Muda haurudi nyuma wala muda hausimami...
Matumizi ya muda ni haya yafuatayo ambayo watu wengi hatuyafati kufikia malengo yetu..
shafiinad.com nakujuza kuwa mwaka huu 2017 ni mwaka wako wa mafanikio kama utatunza muda wako...

1. USIPENDELEE OVER TIME.
Watu wengi walioajiriwa wanapenda sana na huwa wanafurahi sana wakipewa over time yaani kufanyishwa kazi baada ya muda wa kawaida wa kazi wakifurahia kulipwa pesa ya ziada nje ya mshahara wake. lakin kumbe anajimaliza yeye bila kujua ule muda angeenda nyumban kwake au katika miradi yake kama anayo akaiendeleza au akaenda nyumban kwake akaweza kuanzisha mradi wowote ule utakaomsaidia kuingiza pesa kila siku na sio kutegemea over time ya siku moja moja...

2.EPUKA VIJIWE VYA STORY TU.
Watu wengi nikiwemo mimi pia ingawa ilikuwa zamani tunapenda baada ya kazi kupata time ya kwenda vijiweni then tunapiga soga wee mpaka usiku tunarudi nyumbani kulala.
hii hutuathiri sana katika uwezo wa kufikiria maendeleo muda mwingi kwenye story hatupigi story za tufanye nini tutoke huwa tuna piga story za kuchekesha tu lakini muda huo ulitakiwa ukae na ujadili ni namna gani unaweza kujikwamua katika maisha uliyonayo sasa...


3.PUNGUZA KUANGALIA TV NA MITANDAO YA KUCHART.
Mara nyingi watu tunatumia mitandao ya kijamii kupata story,habari mpya na hata kujiongezea maarifa katika maisha yetu lakini katika sehemu ya muda unatakiwa ujiwekee ni muda gani utakuwa wa kuangalia Tv ni muda gani utakuwa wa ku chat na marafiki na muda gani wa kujisomea vitu vitakavyokuongezea maarifa katika maisha yako...
jitahidi muda mrefu au muda mwingi uwe ni wa kujifunza maarifa kwa kusoma makala kama hizi au kusoma vitabu vya kukupa mwanga zaid wa mafanikio...
tembelea blog yangu ya shafiinad.com upate maarifa zaidi...

4.JIWEKEE RATIBA YA KILA SIKU NA HAKIKISHA UNAIFATA.
Ili uweze kumanage muda wako ni lazima uwe na mipango mikakati yako itakayo kuelekeza au kuongoza katika kila jambo unalotakiwa kulifanya katika muda husika hii itakusaidia kutimiza kazi au malengo uliyojipangia kwa siku au mwaka na kupunguza au kuondosha kabisa upotevu wa muda ambao unakugharimu sana katika maisha yako..
wakati wa kupangilia ratiba zako za kila siku cha kwanza ni kuvipa vipao mbele vile vitu vyote vya muhimu ili kuweza kukusaidia wewe kufikia malengo mfano, kuna ratiba ya kwenda kumsalimu rafiki yako na ratiba nyinginee ni ya kwenda afisa kilimo akakupe ushauri wa juu ya kilimo cha umwagiliaji basi ratiba ya kwenda kwa afisa kilimo ndio iwe ya kwanza ikifuatiwa na ya kwenda kumsalimu rafiki...

Kwa leo nadhani hizo ni baadhi ya factor au mawazo niliyonayo juu ya matumizi mazuri ya muda na nadhani na wewe unayo mengi sana zaidi ya haya yangu niliyonayo na unaweza share nasi hapo chini katika sehem ya comments...
karibu shafiinad.com upate kuelimika na kupata nafasi za kujifunza vitu vingi vya maendeleo, teknolojia, afya na mahusiano pia katika jamii zinazotunguka...

Shafii Said Rajabu
MLT
C.E.O of Shafii lab services

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here