KAZI NA FAIDA 5 ZA TUNDA NDIZI KIAFYA - SHAFIINAD

Breaking

TANGAZA NASI

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 1 January 2017

KAZI NA FAIDA 5 ZA TUNDA NDIZI KIAFYANdizi ni tunda ambalo linapatikana kwa wingi sana Tanzania hasa katika mikoa ya nyanda za juu na kwa wastani katika mikoa ya pwani..
 
Zao hili hutumika kama Tunda la kula

 wakati wa kula chakula na pia wakati mwingine hutumika kama chakula hupikwa wakati bado hazijaiva..
Sasa leo hapa shafiinad.com nataka kuzungumzia ndizi mbivu kama tunda na sio chakula..FAIDA/KAZI ZAKE MWILINI

1/ ENERGY BOOST.

Ndizi zina kiwango flani cha sukari katika vitu vilivyomo ndan ambapo huweza kumsaidia mtu aliyechoka kuweza kuapata nguvu wakati akiwa amechoka, mwili hupata nguvu kwa kula vyakula aina ya wanga na wanga huzalisha sukari mwilini ili mwili uweze kuzalisha nguvu kupitia ile sukari iliyozalishwa na Ndizi.

2/ POTASSIUM POWER

Ndizi zina potassium ndani yake pia ambayo hufanya kazi kama hiyo ya sukari lakini hii hasa hustimulate msukumo wa damu kwenye ubongo na kusaidia moyo kuweza kufanya kazi vizur ipasavyo, pia mara kwa mara sio siku zote huweza kupunguza au ku control presha ya damu, pia inasaidia kuzuia muscle clamps(kukaza misuli)  wakati wa mazoez
 
3/ IRON RICH

Ndizi zina kiwango kingi cha madini ya chuma ambapo mtu mwenye upungufu wa madini haya anaweza kula na akarudi katika hali yake ya kawaida ya kuwa na normal level ya iron katika mwili wake ambayo tunajua iron inasaidia katika hemoglobin production.

4/ LOW IN CALORIES

Ndizi ni moja kati ya matunda yanayotumiwa katika kupunguza unene,tumbo na hata mwili kwa ujumla,
Tujuavyo mtu anapokula sana vyakula vyenye calories tuna asilimia kubwa sana ya mtu huyu kuwa mnene(obesity) na kupelekewa kuwa na magonjwa kama presha na sukari kupanda mara kwa mara, sasa ndizi ni tunda ambalo lina calories kiasi.

5/ FIBERS

Tukifuata utafiti wa wamarekani ndizi moja ina uzito wa gram 3 za fibers, Fibers katika mwili wa binadamu zinafanya kazi hasa katika maeneo ya mmeng’enyo wa chakula na kusaidia kazi ya kukisaga chakula kuwa rahisi na kwa wale wenye matatizo ya choo kigumu au kutokupata choo kabisa uweze kuwa na hali nzuri katika upataji choo na choo chako kwa ujumla..
Kwa leo naomba niishie hapa na tutaendelea kupeana zaid maswala ya vyakula vinavyohusika na afya ya binadamu, katika Nyanja za kupunguza magonjwa na matumizi ya dawa za kisasa..
Tembelea shafiinad kila siku kupata habari za afya,fursa,teknolojia,mahusiano pamoja na kilimo.

No comments:

Post a Comment

Nitafurahi sana kama utaweka comment yako hapa chini kwa njia rahisi chagua ANONYMOUS wakati wa kuandika jina ili iwe rahisi we ku comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here